Jiji la Dar es salaam limeripotiwa kutokuwa na mgonjwa yoyote wa kipindupindu kuanzia Desemba mwaka jana.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Naibu waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto Mh. Dkt Hamisi Kigwangalla
amesema kuwa licha ya ugonjwa wa kipindupindu kuanzia jijini Dar es
salaam na kudumu kwa miezi minne lakini kwa sasa hajaripotiwa mgonjwa wa
kipindupindu.
“Mkoa
wa Dar es salaam ambako ndipo ugonjwa ulipoanzia na kudumu kwa miezi
minne haujaripotiwa kuwa mgonjwa wa kipindupindu kuanzia tarehe
22/12/2015,” alisema Kigwangalla.
Waziri
Kigwangalla aliongeza kuwa mikoa mingine ambayo haijaripotiwa kuwa na
maambukizi kwa muda wa wiki moja ni pamoja na
Mbeya,Rukwa,Katavi,Kigoma,Kagera na Lindi.
Aidha
alisema kuwa mikoa ambayo haijarioptiwa ugonjwa huo kwa zaidi ya miezi
miwili iliyopita ni Shinyanga, Kilimanjaro na Iringa pia amesema kuwa
kuna mikoa ambayo haijawahi kuripoti tangu ugonjwa wa kipindupindu uanze
nayo ni mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mtwara.
Dkt.
Kigwangalla alitaja mikoa iliyotoa idadi kubwa ya wagonjwa wa
kipindupindu ambayo ni Halmashauri ya Morogoro(66), Arusha (50),
Singida(40), na manispaa ya Dodoma (33).
Pia
amewaasa wananchi kunywa maji yaliyo safi na salama, kuepuka kula
chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na salama pamoja na
kunawa mikono na maji safi na sabuni kwa maji safi yanayotiririka
pamoja na kutumia vyoo wakati wote na kutokujisaidia ovyo katika vyanzo
vya maji ,maziwa na mabwawa.
Kwa
mujibu wa wizara ya afya tangu ugonjwa wa kipindupindu uanze, jumla ya
watu 13,491 wameugua kipindupindu, na kati yao watu 205 wameshafariki
kutokana na ugonjwa huo.
0 comments:
Post a Comment