CHAMA
cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimeelezea kuridhishwa kwake na maamamuzi
ya Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa kutangaza siku ya kufanyika kwa
uchaguzi wa marudio kwa nafasi ya Urais, Uwakilishi na Udiwani.
Kimesema
maamuzi ya kufanyika uchaguzi huo Machi 20 mwaka huu, yanaenda
sambamba na matakwa ya wananchi waliokuwa wengi katika kutekeleza haki
yao ya kidemokrasia kwa mujibu wa miongozo ya katiba ya Zanzibar ya
mwaka 1984.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Itikadi
na Uenezi CCM Zanzibar, Waride Bakar Jabu alisema kwamba CCM inaungana
na vyama vingine vya kisiasa nchini vilivyobaini kasoro za uchaguzi mkuu
uliopita kuwa na kasoro na kuunga mkono maamuzi ya ZEC kuwa ni sahihi
kwani yamefuata hatua muhimu za Kikatiba.
Waride
alisema msimamo wa CCM katika Mkwamo wa kisiasa uliopo Zanzibar ni
kurudi katika uchaguzi wa marudio ili kila chama cha kisiasa
kinachoshiriki katika uchaguzi uliopita kipate haki ya kungia madarakani
kwa njia halali na zinazokubalika kisheria.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo Waride alieleza kwamba maamuzi hayo ndiyo
kipimo sahihi cha kuweka uzani wa ukomavu wa kisiasa na demokrasia
katika mfumo wa vyama vingi kwani lazima kila chama chenye haki ya
kushiriki katika uchaguzi kiridhike na hatua zote zinazofanywa mpaka
kupatikana kwa mshindi anayeongoza kwa wingi wa kura halali.
“
Tunachukua fursa hii kuwaomba wananchi wote wenye haki ya kupiga kura
hasa wafuasi wa CCM pamoja na wananchi wote wajitokeze kwa wingi kwenda
kupiga kura Machi 20 mwaka huu.
"Tukumbuke
kwamba maamuzi hayo yamefanywa na Chombo chenye Mamlaka ya kusimamia
masuala yote ya Uchaguzi nchini baada ya kujiridhisha kuwa kuna kasoro
zilizotokea katika uchaguzi uliofutwa na kuona kuna haja ya kila
mwananchi kupata haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka kwa njia huru,
wazi na zinazokubalika kisheria”. Alifafanua Waride na kuongeza kuwa uchaguzi huo ndiyo njia mwafaka ya kumaliza mkwamo wa kisiasa Zanzibar.
Katibu
huyo aliongeza kwamba pia wanaunga mkono msimamo wa vyama vya vyote vya
kisiasa vilivyokubali kushiriki uchaguzi wa marudio pamoja ushauri wa
Msajili wa Vyama vya Sisasa nchini, Francis Mtungi kwa kuvitaka vyama
vyenye usajili kushiriki katika mchakato huo ili kudumisha Demokrasia na
malengo na malengo ya vyama kutumia uchaguzi kushika Dola.
Akizungumzia
suala la CUF kususia Uchaguzi wa marudio alisema kwamba walichofanya ni
mwendelezo wa migomo na kususa kwa mipango ya maendeleo inayofanywa na
mamlaka za serikali katika kufanya mipango mbali mbali ya maendeleo kwa
maslahi ya wananchi, hivyo hakuna jipya wala athari inayoweza kuathi
hali ya kisiasa Zanzibar.
Alisema
kwamba upinzani wa aina hiyo hauna nia njema ya kujenga maendeleo ya
nchi bali una nia malengo ya kukwamisha na kudumaza maendeleo ya nchi
kwa maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaoweka mbele
tamaa ya madaraka kuliko maisha ya wananchi.
“
Kila chama kina sera zake na misimamo yake sasa wao kama wameona
kususia uchaguzi wa marudio ndiyo njia ya kumaliza mkwamo wa kisiasa
Zanzibar hiyo ni juu yao, lakini sisi tutashiriki kikamilifu ili chama
chetu kipate ridhaa ya wananchi kurudi madarakani ya kidemokrasia."
Aidha
alisema chama hicho kinaamini kwamba Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba
25 mwaka 2015 ulikuwa na kasoro nyingi zilizosababisha uchaguzi huo
kukosa sifa ya kuwa uchaguzi huru na wa haki na hatimaye kufutwa.
Kupitia
taarifa hiyo Waride wamewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika
mkutano wa hadhara wa mikoa minne kichama ya Unguja katika uzinduzi wa
miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM itakayofanyika katika Afisi kuu ya CCM
Kisiwandui, January 31 mwaka huu.
Alisema
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Makamo Mwenyekiti wa
CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein
0 comments:
Post a Comment