Monday, 28 September 2015

#YALIYOJIRI>>>Tanga yavunja rekodi ya mafuriko waanzisha Hurricane mkoani Tanga haijawahi.Jionee hapa.

 Tanga wakiwa tayari kuyakubali mabadiliko ,viwanja vya Tangamano leo Jumatatu 28/9/2015
 Tanga wakiwa tayari kuyakubali mabadiliko ,viwanja vya Tangamano leo Jumatatu 28/9/2015
  Tanga wakiwa tayari kuyakubali mabadiliko ,viwanja vya Tangamano leo Jumatatu 28/9/2015
 
  Tanga wakiwa tayari kuyakubali mabadiliko ,viwanja vya Tangamano leo Jumatatu 28/9/2015
  Tanga wakiwa tayari kuyakubali mabadiliko ,viwanja vya Tangamano leo Jumatatu 28/9/2015
Kijana wa kitanga akiwa tayari kwa Mabadiliko baada ya Kujiandika Mgongoni.


Sunday, 27 September 2015

#MICHEZO>>>Nahodha wa Azam FC azalilishwa.Fahamu zaidi hapa.


Timu ya Azam September 27 ikiwa katika uwanja wake wa Azam Complex Mbande Chamazi akicheza mechi  yake na Mbeya City,nahodha wa Mbeya City Juma Nyoso alimfanyia kitendo cha kidhalilishaji nahodha  wa Azam FC John Bocco, licha ya kuwa muamuzi hakuona ila kupitia picha za mnato na kanda za video tukio hilo lilinaswa na kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Toa maoni yako ukiwa mpenzi wa michezo.

#YALIYOJIRI>>>Mgombea Urais CHADEMA UKAWA Edward Lowassa,akiwahutubia wananchi wa Mji wa Himo.Fahamu zaidi hapa.


 Mgombea Urais CHADEMA UKAWA Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Himo Kwenye mkutano wa kampeni
 Mgombea Urais CHADEMA UKAWA Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Himo Kwenye mkutano wa kampeni
 Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, akiwahutubia Umati wa wananchi Himo na kumnadi Mgombea Urais UKAWA Edward Lowass
James Mbatia akimpokea Edward Lowassa viwanja vya Oria shule ya msingi Kahe leo J/pili 27/9/2015

#MCHEZO>>Yanga FC,Azam na Mtibwa zang'ang'ania tatu bora ligi kuu Tanzania Bara.Fahamu zaidi hapa.

Date / Time Home Results Away Season League
09/27/2015 - 00:00 African Sports 1 - 0 Ndanda FC 2015-2016 Premier League
09/27/2015 - 00:00 Azam FC 2 - 1 Mbeya City Council FC 2015-2016 Premier League
MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA BAADA YA MICHEZO YA 27SEPTEMBER2015.
Pos Club P W D L GF GA GD PTS
1 Young Africans SC 4 4 0 0 11 1 10 12
2 Azam FC 4 4 0 0 7 2 5 12
3 Mtibwa Sugar FC 4 4 0 0 6 1 5 12
4 Simba SC 4 3 0 1 6 3 3 9
5 Stand United 4 2 0 2 3 3 0 6
6 Majimaji FC 4 2 0 2 2 2 0 6
7 Tanzania Prisons 4 2 0 2 3 5 -2 6
8 Toto African 4 1 2 1 1 2 -1 5
9 Mwadui FC 4 1 1 2 2 2 0 4
10 Ndanda FC 4 1 1 2 3 4 -1 4
11 JKT Mgambo 4 1 1 2 2 4 -2 4
12 Kagera Sugar FC 4 1 1 2 2 4 -2 4
13 Mbeya City Council FC 4 1 0 3 4 4 0 3
14 African Sports 4 1 0 3 1 5 -4 3
15 Coastal Union SC 4 0 2 2 0 3 -3 2
16 JKT Ruvu Stars 4 0 0 4 1 9 -8 0

#MICHEZO>>>Azam yaendeleza ushindi baada kuifunga Mbeya City.Fahamu zaidi hapa.

Azam FC yaendeleza wimbi la ushindi  katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa mabao 2-1 Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mchezo huu ulioharibiwa na maamuzi ya hovyo ya Martin Saanya wa Morogoro, aliyesaidiwa na Julius Kasitu wa Shinyanga na Sylvester Mwanga wa Kilimanjaro, hadi mapumziko Azam FC walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Kiungo Mudathir Yahya Abbas aliifungia Azam FC bao katika dakika ya 10 baada ya kuuwahi mpira uliookolewa kufuatia yeye mwenyewe kupiga shuti na lililookolewa kabla wa kuuwahi mpira na kufunga.
Timu zote zilishambuliana kwa zamu kipindi cha kwanza na Mbeya City walipoteza nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 44 baada ya shuti la Joseph Mahundi kugonga mwamba na kurudi uwanjani na kumkuta Serge Wawa Pascal aliyeokoa.
Kipindi cha pili, mchezo uliendelea kuwa wa staili ile ile, timu zote kushambuliana kwa zamu.


Mshambuliaji Kipre Herman Tchetche kutoka Ivory Coast aliifungia Azam FC bao la pili dakika ya 52 akimalizia pasi ya Sure Boy.
Mbeya City walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Raphael Alpha dakika ya 56.
 
Kipre Tchetche aliifungia Azam FC bao ambalo lingekuwa la tatu, lakini refa Saanya akasema mfungaji aliotea.
Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ifikishe pointi 12, sawa na Mtibwa Sugar na Yanga SC, zikifuatiwa na Simba SC yenye pointi tisa.

Kikosi  cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, David Mwantika, Racine Diouf, Serge Wawa Pascal, Jean Baptiste Mugiraneza, Mudathir Yahya/Himid Mao dk46, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco, Kipre Tchetche/Alan Wanga dk78 na Farid Mussa. 
Mbeya City; Hannington Kalyesebula, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Juma Nyosso, Christian Sembuli, Steven Mazanda, Richard Peter, Raphael Alpha, George Mlawa/David Kambole dk85, Themi Felix/Meshack Samuel dk58 na Joseph Mahundi. 

#YALIYOJIRI>>>Wananchi wa Makambako wakiwa tayali kumpokea mgombea wa CCM Magufuli baada ya kuwasili.

 Watu wakionyesha Nyuso za furaha punde baada ya mgombea kuwasili
 Makambako, Mafinga na Mbarali Magufuli alizungumza na wakazi hao kwa mida tofauti leo tar 27 September 2015.
  Watu wakionyesha Nyuso za furaha punde baada ya mgombea kuwasili
  Mama akionyesha Nyuso ya furaha punde baada ya mgombea kuwasili
 Watu wakionyesha Nyuso za furaha punde baada ya mgombea kuwasili

Saturday, 26 September 2015

#YALIYOJIRI>>>Mtu mmoja amekufa papo baada ya TASHRIFF kuligonga gari dogo.Fahamu zaidi hapa.

Mtu mmoja amekufa papo hapo na wengine wanne wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya TASHRIFF lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dodoma kuligonga gari dogo aina ya Nissan Safari katika eneo la kange jijini Tanga.
Akizungumza katika eneo la tukio dereva wa gari dogo ANDREW LIMONGA amesema dereva wa basi la TASHRIFF,MOHAMED JUMAA ambaye ndiye pekee aliyefariki dunia katika ajali hiyo hakufunga mkanda.
Amesema basi la TASHRIFF liliigonga gari yale kwa nyuma na alipoyumba akagongwa tena upende wa kulia ndipo magari yote mawili yalipoteza mwelekeo na kuanguka.
 Chanzo
                                           ITV HABARI

#YALIYOJIRI>>>>Edward Lowassa na Freeman Mbowe wapokelewa na Wananchi wa Boma Hai kwa mabango.Jionee hapa.

Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya Chadema UKAWA Edward Lowassa nasema hivi "Watanzania wana imani na mimi pamoja na viongozi wenzangu wataungana nasi kupambana na umaskini wa nchi hii".

MICHEZO ILIYOCHEZWA LEO LIGI KUU TANZANIA BARA NA MSIMAMO YAKO HAPA.

Saturday 26/09/2015
 MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA BAADA YA MICHEZO YA Saturday 26/09/2015
Pos Club P W D L GF GA GD PTS
1 Young Africans SC 4 4 0 0 11 1 10 12
2 Mtibwa Sugar FC 4 4 0 0 6 1 5 12
3 Azam FC 3 3 0 0 5 1 4 9
4 Simba SC 4 3 0 1 6 3 3 9
5 Stand United 4 2 0 2 3 3 0 6
6 Majimaji FC 4 2 0 2 2 2 0 6
7 Tanzania Prisons 4 2 0 2 3 5 -2 6
8 Ndanda FC 4 1 2 1 3 3 0 5
9 Toto African 4 1 2 1 1 2 -1 5
10 Mwadui FC 4 1 1 2 2 2 0 4
11 JKT Mgambo 4 1 1 2 2 4 -2 4
12 Kagera Sugar FC 4 1 1 2 2 4 -2 4
13 Mbeya City Council FC 3 1 0 2 3 2 1 3
14 Coastal Union SC 4 0 2 2 0 3 -3 2
15 African Sports 4 0 1 3 0 5 -5 1
16 JKT Ruvu Stars 4 0 0 4 1 9 -8 0
 

#MICHEZO>>>Yanga FC yaonesha Ubora wao mbere ya watani wao Simba FC hiyo jana.Fahamu zaidi hapa.

Timu ya Yanga FC Baada ya kukosa ushindi kwa kipindi cha miaka kadhaa hatimaye leo  wamewafunga watani zao wa  Simba FC kwa ushindi wa goli 2-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara wa raundi ya nne ulipigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Amis Tambwe na Malimi Busungu wameibuka mashujaa kwenye mchezo wa leo lakini sifa pekee zinaenda kwa Busungu aliyeingia kipindi cha kwanza kuchukua nafasi ya Msuva na kutengeneza bao lililofungwa na Tambwe dakika ya 44 kipindi cha kwanza kabla ya yeye kufunga bao la pili dakika ya 79 kipindi cha pili.
Simba FC watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kufunga mabao kipindi cha kwanza wakati wanatawala mchezo kabla ya mambo hayajawa magumu baadae walipofungwa.

Mpira ulianza kwa kasi huku Simba wakitawala sana sehemu kubwa ya mchezo na mara nyingi walitengeneza mashambulizi lakini safu ya ushambuliaji iliyokuwa inaongozwa na Hamis Kiiza pamoja Mussa Mgosi ilishindwa kutumia nafasi hizo kufunga magoli.

Muda mwingi wa kipindi cha kwanza Yanga walikuwa wakishambuliwa huku Simba wakitengeneza mashambulizi yao kupitia upande wa winga ya kulia na kumpa Haji Mwinyi kazi ya ziada.
Baada ya kuonekana mchezo umemkataa Simon Msuva, kocha wa Yanga alifanya mabadiliko ndani ya kipindi cha kwanza kwa kumtoa Msuva na nafasi yake ikachukuliwa na Malimi Busungu ambaye alionesha uhai mkubwa na badae kutoa pasi ya goli lililofungwa na Amis Tambwe.

Kipindi cha pili mambo yaligeuka baada ya Yanga kumiliki mchezo na kufanya mashabulizi kadhaa kwenye lango la Simba yaliyokuwa na madhara.

MICHEZO ILIYOCHEZWA LEO LIGI KUU UINGEREZA NA MSIMAMO YAKO HAPA.


MSIMAMO WA LIGI KUU UINGEREZA BAADA MICHEZO YA LEO.
POS
LP CLUB P W D L GF GA GD PTS
1 (2) Manchester United 7 5 1 1 12 5 7 16
2 (1) Manchester City 7 5 0 2 13 6 7 15
3 (3) West Ham United 7 4 1 2 15 9 6 13
4 (5) Arsenal 7 4 1 2 10 7 3 13
5 (9) Tottenham Hotspur 7 3 3 1 9 5 4 12
6 (4) Leicester City 7 3 3 1 15 14 1 12
7 (13) Liverpool 7 3 2 2 7 9 -2 11
8 (6) Everton 6 2 3 1 8 5 3 9
9 (16) Southampton 7 2 3 2 10 9 1 9
10 (8) Crystal Palace 6 3 0 3 8 7 1 9
11 (7) Swansea City 7 2 3 2 8 8 0 9
12 (10) Watford 6 2 3 1 5 5 0 9
13 (11) Norwich City 7 2 3 2 11 12 -1 9
14 (12) West Bromwich Albion 6 2 2 2 4 6 -2 8
15 (15) Chelsea 7 2 2 3 11 14 -3 8
16 (14) Bournemouth 7 2 1 4 9 11 -2 7
17 (18) Stoke City 7 1 3 3 7 10 -3 6
18 (17) Aston Villa 7 1 1 5 8 12 -4 4
19 (19) Newcastle United 7 0 3 4 5 11 -6 3
20 (20) Sunderland 7 0 2 5 6 16 -10 2
POS
LP CLUB P W D L GF GA GD PTS