Azam FC yaendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuichapa
mabao 2-1 Mbeya City kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es
Salaam.
Mchezo huu ulioharibiwa na maamuzi ya hovyo ya Martin Saanya wa
Morogoro, aliyesaidiwa na Julius Kasitu wa Shinyanga na Sylvester Mwanga
wa Kilimanjaro, hadi mapumziko Azam FC walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kiungo Mudathir Yahya Abbas aliifungia Azam FC bao katika dakika ya
10 baada ya kuuwahi mpira uliookolewa kufuatia yeye mwenyewe kupiga
shuti na lililookolewa kabla wa kuuwahi mpira na kufunga.
Timu zote zilishambuliana kwa zamu kipindi cha kwanza na Mbeya City
walipoteza nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 44 baada ya shuti la Joseph
Mahundi kugonga mwamba na kurudi uwanjani na kumkuta Serge Wawa Pascal
aliyeokoa.
Kipindi cha pili, mchezo uliendelea kuwa wa staili ile ile, timu zote kushambuliana kwa zamu.
Mshambuliaji Kipre Herman Tchetche kutoka Ivory Coast aliifungia Azam FC bao la pili dakika ya 52 akimalizia pasi ya Sure Boy.
Mbeya City walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Raphael Alpha dakika ya 56.
Kipre Tchetche aliifungia Azam FC bao ambalo lingekuwa la tatu, lakini refa Saanya akasema mfungaji aliotea.
Matokeo hayo yanaifanya Azam FC ifikishe pointi 12, sawa na Mtibwa Sugar na Yanga SC, zikifuatiwa na Simba SC yenye pointi tisa.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, David
Mwantika, Racine Diouf, Serge Wawa Pascal, Jean Baptiste Mugiraneza,
Mudathir Yahya/Himid Mao dk46, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco,
Kipre Tchetche/Alan Wanga dk78 na Farid Mussa.
Mbeya City; Hannington Kalyesebula, John Kabanda, Hassan Mwasapili,
Juma Nyosso, Christian Sembuli, Steven Mazanda, Richard Peter, Raphael
Alpha, George Mlawa/David Kambole dk85, Themi Felix/Meshack Samuel dk58
na Joseph Mahundi.
0 comments:
Post a Comment