Timu ya Yanga FC Baada ya kukosa ushindi kwa kipindi cha miaka kadhaa hatimaye leo
wamewafunga watani zao wa Simba FC kwa ushindi wa goli 2-0
kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara wa raundi ya nne ulipigwa kwenye
uwanja wa Taifa.
Amis Tambwe na Malimi Busungu wameibuka mashujaa kwenye
mchezo wa leo lakini sifa pekee zinaenda kwa Busungu aliyeingia kipindi
cha kwanza kuchukua nafasi ya Msuva na kutengeneza bao lililofungwa na
Tambwe dakika ya 44 kipindi cha kwanza kabla ya yeye kufunga bao la pili
dakika ya 79 kipindi cha pili.
Simba FC watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kufunga mabao kipindi
cha kwanza wakati wanatawala mchezo kabla ya mambo hayajawa magumu
baadae walipofungwa.
Mpira ulianza kwa kasi huku Simba wakitawala sana sehemu
kubwa ya mchezo na mara nyingi walitengeneza mashambulizi lakini safu ya
ushambuliaji iliyokuwa inaongozwa na Hamis Kiiza pamoja Mussa Mgosi
ilishindwa kutumia nafasi hizo kufunga magoli.
Muda mwingi wa kipindi cha kwanza Yanga walikuwa
wakishambuliwa huku Simba wakitengeneza mashambulizi yao kupitia upande
wa winga ya kulia na kumpa Haji Mwinyi kazi ya ziada.
Baada ya kuonekana mchezo umemkataa Simon Msuva, kocha wa
Yanga alifanya mabadiliko ndani ya kipindi cha kwanza kwa kumtoa Msuva
na nafasi yake ikachukuliwa na Malimi Busungu ambaye alionesha uhai
mkubwa na badae kutoa pasi ya goli lililofungwa na Amis Tambwe.
Kipindi cha pili mambo yaligeuka baada ya Yanga kumiliki
mchezo na kufanya mashabulizi kadhaa kwenye lango la Simba yaliyokuwa na
madhara.
0 comments:
Post a Comment