Viongozi wote wa CCM wa kata ya mkomazi na pamoja na wapiga kura
1,400 wa eneo hilo wilayani Korogwe wamejiunga na CHADEMA huku baadhi
yao wakiamua kugombea nafasi mbali mbali za uongozi kwa tiketi ya chama
hicho.
Wakizungumza katika mkutano wa kampeni ulifanyika katika kijiji cha
mikocheni kilichopo kata ya mkomazi wilayani Korogwe baadhi ya viongozi
hao pamoja na wengine wa CCM katika kata sita waliokatwa majina yao
katika zoezi la kura za maoni kwa tiketi ya CCM wamesema wameamua
kujiunga na chadema pamoja na wapiga kura wao ili kuongeza nguvu kupata
wawakilishi wa wananchi katika baraza la madiwani la halmashauri ya
wilaya ya Korogwe.
Kwa upande wake katibu wa CHADEMA jimbo la Korogwe Bwana.Salim
Sempoli amemuomba mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi jimbo la
Korogwe kuharakisha malalamiko ya wapiga katika baadhi ya vituo ambapo
sehemu kubwa ya majina ya wapiga kura katika jimbo la Korogwe vijijini
hayaonekani na hadi sasa hakuna utaratibu uliofanywa kusaidia tatizo
hilo kwa sababu linaweza kuleta viashiria vya uvunjifu wa amani wakati
wa zoezi la kupiga kura.
Kufuatia hatua hiyo mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema Emmanuel
Kimea amewataka wananchi kuwachagua viongozi wa chama hicho kuanzia
ngazi ya taifa,ubunge na udiwani kwa sababu ndani9 ya chama kikoja
changamoto zinazowakabili katika kata ya mkomazi ikiwemo ya migogoro ya
ardhi haiwezi kumalizika kama hawatafanya mabadiliko.
Chanzo
ITV
0 comments:
Post a Comment