Mfuko
wa Bima ya Afya nchini (NHIF) umeingia makubaliano ya udhamini wa bima
ya afya kwa wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi kwa vilabu 16 vya
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja.Akiongea
na waandishi wa habari katika mkutano uliofnayika leo ofisi za TFF
zilizopo Karume, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine amesema
wanaishukuru NHIF kwa kuwapa udhamini huo ambao utavisaidia vilabu vya
Ligi Kuu katika matibabu ya wachezaji na bechi ka ufundi.Tumekua
na kilio cha muda mrefu juu ya vilabu vya Ligi Kuu kuwa na Bima za afya
kwa wachezaji, kitu ambacho kipo kikanuni lakini vilabu vilikuwa
vinashindwa kutimiza hitaji hilo la kikanuni na sasa TFF kwa kushirikian
na NHIF tutakua tumeiondoa tatizo hilo.Naye
Mkuu wa Mawasiliano wa NHIF, Sungi amesema udhamini huo wa bima ya
matibabu kwa wachezaji na benchi la ufundi utatolewa kwa matibabu yote
yatakayofnayika ndani ya nchi.Toa maoni yako hapa.
0 comments:
Post a Comment