Monday, 21 November 2016

#MICHEZO>>>>SIMBA YAITISHA MKUTANO WA DHARURA, UTAFANYIKA DESEMBA 11.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Uongozi wa klabu ya Simba umeitisha mkutano wa wanachama wa dharura utakaofanyika Desemba 11.

Mkutano huo umeitishwa baada ya kikao cha kamati  ya utendaji wa klabu hiyo iliyokaa juzi. Mkutano huo utafanyika kwenye Ukumbi wa Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema kamati ya utendaji imetoa baraka zake kupitia ibara ya 22 ya katiba ya Simba.


“Mkutano huo utakuwa ni mwendelezo wa mkutano wa kawaida uliofanyikaJulai 31, 2016,” alisema Manara.
Ingawa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari haijafungua kila kitu, lakini inaonekana mwendelezo utakuwa ni ule kuhusiana na kuboresha suala la uongozi Simba na kuingia katika suala la uwekezaji kama ambavyo mfanyabiashara Mohammed Dewji alivyojitokeza.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

#MICHEZO>>>>RONALDO ANAREJEA URENO KESHO NA KIATU MAALUM CHENYE TAREHE SIKU FERGUSON ALIPOMUITA MAN UNITED.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Kesho Jumanne, Real Madrid itakuwa genii dimbani ikiivaa Sporting Lisbon katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Cristiano Ronaldo atakuwa na raha zaidi kwa kuwa atakuwa anarejea nyumbani tena, lakini safari hii akiwa na kiatu maalum.
Viatu hivyo vimetengenezwa na Nike vikiwa na tarehe maalum inayoonyesha Agosti 6, 2003.

Agosti 6, 2003 ndiyo siku maisha ya Ronaldo yalipobadilika katika uwanja atakaocheza Jumanne wakati Manchester United walipocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Sporting Lisbon.

Baada ya mechi hiyo, Man United wakiwa wamelala kwa mabao 3-1, Kocha Alex Ferguson alimueleza Ronaldo kwamba anamhitaji ajiunge na Man United.


Mwaka 2009 aliondoka United na kujiunga Real Madrid ambayo kesho anakwenda nayo mjini humo.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

#YALIYOJIRI>>>Rais Magufuli akutana na kiongozi wa Jeshi la Ukombozi la China.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 21 Novemba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni Kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong, Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Viongozi hao wamezungumzia uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na China katika nyanja mbalimbali ikiwemo katika masuala ya ulinzi ambapo Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) limekuwa na ushirikiano na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA)
 
Rais Magufuli amemueleza Jenerali Fan Changlong kuwa Tanzania inathamini ushirikiano huo ambao umechangia kufanikisha juhudi za kuimarisha JWTZ zinazolenga kuwa na Jeshi la Kisasa na vifaa bora.
 
Dkt. Magufuli amemuomba Jenerali Fan Changlong afikishe salamu na shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping na kumhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na China katika kuimarisha majeshi ya ulinzi na pia katika masuala mengine ya maendeleo ya kijamii.
 
“Nimefurahishwa na ziara yako hapa nchini kwetu, ujio wako unazidi kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi zetu ulioasisiwa na waasisi wa mataifa haya Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Hayati Mwenyekiti Mao Tse-tung wa China.
 
“Naomba unipelekee salamu zangu kwa Rais Xi Jinping na umwambie kuwa pamoja na kuendeleza uhusiano na ushirikiano wetu katika kuimarisha majeshi pia tunatarajia kuona China inakuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi zetu za maendeleo kwa kujenga viwanda na kushiriki katika miradi mingine ukiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani Standard Gauge” amesema Rais Magufuli.
 
Kwa upande wake Jenerali Fan Changlong amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi imara aliouonesha katika Awamu ya Tano na amemhakikishia kuwa China itaendeleza na kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania katika masuala ya usalama hasa kuimarisha JWTZ.
 
Jenerali Fan Changlong amesema Jeshi la Ukombozi la Wananchi wa China na Jeshi la Wananchi Tanzania yana uhusiano wenye manufaa makubwa na kwamba hivi sasa yanafanya uboreshaji utakaoyaimarisha zaidi na kuwa majeshi ya kisasa.
 
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na Makamanda wa Majeshi wa Tanzania na China.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kwa mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong wakati wakelekea kwenye ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na ujumbe wake akiongoza mazungumzo rasmi na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Watu wa China(PLA) pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Maafisa wa ngazi za juu katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ.
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
21 Novemba, 2016

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

#BURUDANI>>>HATIMAYE TAMASHA LA FIESTA LAPATA MPINZANI….DIAMOND AANZISHA TAMASHA LAKE..KUMLETA STAR HUYU WA MAREKANI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

 Katika kusherehekea Christmas mwaka huu, WCB wanatarajia kufanya show yao ya kwanza wakiwa pamoja, December 24 iliyopewa jina Wasafi Beach Party jijini Dar es Salaam.
Wasanii wote wa label hiyo wakiongozwa na Diamond watatumbuiza. Lakini huenda kukawa na ugeni mkubwa wa staa wa nje na tayari meneja wa Diamond, Sallam ametease jina.

Akiweka picha ya mrembo wa Marekani, Amber Rose, Sallam ameandika kwenye Instagram, “Wangapi watu wanataka huyu dada ashuke bongo siku akinukishe watu wale nae Bata???”
Naye Diamond alichombeza kwenye post yake: Eti Manager @sallam_sk anauliza wangapi wangependa huyu dada @amberrose siku ashuke Bongo watu wale nae Bata???”

Huenda label hiyo ikawa imepanga kumleta mrembo huyo kuwa host wa tamasha lenyewe.

Hiyo haitakuwa mara ya kwanza kwa ex huyo wa Wiz Khalifa kuja Afrika. Mwaka jana alienda Lagos, Nigeria kwa mwaliko wa D’Banj ambako hata hivyo alikaa jukwaani kwa dakika 7 tu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

#YALIYOJIR>>>>Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kasulu Mjini(NCCR) na kuhamia ACT-Wazalendo, Moses Machali ahamia CCM.Fahamu zaidi hapa.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE. ​

Kutoka mezani kwangu Moses Joseph Machali, Tarehe: 21/11/2016

Napenda kuutaarifu umma wa Watanzania kupitia kwenu waandishi wa habari kwamba ni jambo la ajabu na aibu kwa watu makini na wenye kuhitaji mabadiliko ya kweli Kuacha kuunga Mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini Uongozi wa Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli bila kusahau utendaji makini wa Waziri Mkuu wake Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa (Mb) pamoja na mawaziri mbalimbali wameonesha kutaka kufuata mwenendo wa Rais Magufuli na Waziri Mkuu wake.

Mimi Moses Joseph Machali niliyefanya sana siasa za Upinzani hapa nchini na niliyepiga kelele na kupinga siasa za kifisadi zilizoitawala nchi hii; niliyepinga pia ufisadi uliokuwa umeitawala serikali huko nyuma kwa nguvu na uwezo wangu wote nikishirikiana na wapinzani wenzangu, ninaamua kujiunga na watu wanaonesha dhamira safi ya kuiendeleza nchi yetu Tanzania. Watu wenye mwelekeo na dhamira ya kuijenga nchi yetu kwa maendeleo enedelevu ni jamii ya akina Magufuli, Kasim Majaliwa, nk.

Mwaka mmoja wa Uongozi wa Rais Magufuli na baadhi ya wasaidizi wake kupitia hatua mbalimbali zilizochukuliwa dhidi ya ufisadi uliokuwa umeigubika nchi yetu, inatosha kabisa kwa mtu yeyote makini kufanya uamuzi wa kumuunga mkono au kutokumuunga mkono Rais Magufuli.

Mimi nimechagua kumuunga Mkono Rais kwa vitendo, kwa sababu ninaposoma Rekodi yangu ya enzi nikiwa Mbunge (Hansard) na kabla ya kuwa mbunge ni kwamba nilipinga mnoo wizi na ufisadi wa kila aina; Nilipinga Matumizi ya fedha serikalini yasiyo ya lazima na yasiyo na tija kwa taifa (Rejeeni hotuba yangu ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi, nikiwa Waziri Kivuli wa wizara hiyo ya mwaka 2014/2015 na 2015/2016), vilevile bila kusahau hotuba zangu mbalimbali Bungeni na nje ya Bunge.

Kwa kushirikiana na wapinzania wenzangu enzi hizo tulishauri na kupinga ufisadi wa kila aina, tuliitaka serikali kufanya mambo yenye tija kwa taifa na sasa kila mwenye macho anaona hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano. Miradi kama ya Ujenzi wa Reli, Ununuzi wa ndege mbili na mipango ya kununua ndege zaidi kama namna ya kulifufua shirikia la ATCL ni mambo tuliyoyahitaji kuyaona wapinzani; sasa yanafanyika. Wale wenye dhamira ya dhati ya kuona nchi yetu ikipiga hatua, kamwe hatuwezi kubeza mambo hayo bali kuyaunga mkono.

Wale tuliosema na kupiga kelele kwamba Serikali ni dhaifu ktk kuwachukulia hatua watu mbalimbali wenye dhamana serikalini walioonekana kufanya vibaya serikalini ktk nafasi zao, leo tunaona kumekuwepo na kasi nzuri ktk kuwachukulia hatua watu hao. Hata hivyo leo hii upinzani umepiteza mwelekeo kwa sababu unapingana na kile ulichokihubiri nchini.

Agenda ya kupinga ufisadi siyo ya upinzani tena bali ya JPM na CCM yake au yao. Wapinzani wamegeuka kuwa watu wanaokataa yale waliyoyasimamia na kuyahubiri huko nyuma. Hakika huo siyo uungwana bali aina mpya ya ufisadi nchini na usaliti kwa agenda zao.

Kama kweli sisi tumeokuwa wapinzani na tulioonesha kupinga kwa nguvu zote ufisadi ulioiumiza nchi hii tulimaanisha yale tuliyoyahubiri na kuwaaminisha watu basi tunao wajibu wa kuacha tabia ya kuwa vigeugeu kwa mambo tuliyoyaamini na kuyahubiri. Kutofanya hivyo basi ni mwendelezo wa ufisadi kwa maslahi binafsi.

Ni nani asiyeona kwamba serikali ya awamu ya tano inafanyia kazi mambo mengi tuliyoyapigia kelele? Au tunajifanya kutokukubali ukweli unaoishi kwa ule msingi wa upinzani wa Tanzania kwamba Tukimuunga mkono Mtawala kamwe hatutapata kuaminiwa na wapiga kura nchini na hivyo tupinge tu hata kama ni ukweli? Nadhani kinachofanyika ni mwendelezo wa kupinga hata mazuri ili kutafuta fursa ya wapinzani kukubalika kisiasa zaidi hata kwa njia na mbinu haramu kama kawaida ya siasa zilizo zoeleka hapa nchini kwa miaka mingi.

Taifa hili haliwezi kuendelea kwa kuwa na siasa za kutokukubaliana na ukweli unaoishi. Kama dhamira ya kila mtanzania ikiwemo wapinzani ni kuona nchi ina move basi hatuhitaji kuwa watu wa kupingapinga hata yaliyo mema bali kuyaunga mkono yale yaliyo mema bila kujali yanafanywa na nani bali msingi mzuri unapaswa kuwa ukweli kwa kila jambo.

Serikali ya awamu ya tano imeonesha njia ktk mambo mengi na inastahili kuungwa mkono. Safari ni hatua na ninaamini kwamba hata yale yanayoonekana kutokufanyiwa kazi ndani ya mwaka mmoja uliopita na ambayo yalishindikana huko nyuma, bado yanaweza kuja kufanyiwa kazi huko mbeleni. Serikali ya JPM imejitahidi sana tukilinganisha na huko tuliko toka. Uongozi huu unafanana sana na ule wa akina Hayati EDAWARD MORINGE SOKOINE chini ya hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere.

Daima ninaamini ktk yale ninayoyaamini pasipo kufungwa na ukada bali kuangalia ukweli ni upi. Hata kelele wanazopiga baadhi ya watu kwamba maisha yamekuwa magumu kwa sababu ya Magufuli ni propaganda tu kwa sababu hakuna uhusiano wa maisha magumu na suala la KUDHIBITI wapiga dili wa fedha na mali za umma bali tukubali kwamba wapiga dili waliozoea kupiga dili na kuziingiza fedha walizopiga ktk mzunguko kwamba siyo jambo la msingi ktk kujenga uchumi imara.

Uchumi imara hauwezi kujengwa kwa kuruhusu ubadhirifu wa fedha na mali za umma au hata za mtu mmoja mmoja. Kinachoonekana hivi sasa ni kama nchi inasukwa upya na hivyo tuwaunge mkono viongozi wa serikali ya awamu ya tano kwa mema wanayoyafanya na kuwashauri kurekebisha ktk yale ambayo hayajakaa vizuri. Tuachane na siasa nyepesi za kutaka kuona kwamba mazuri ni yale yanayofanywa na wapinzani huku mambo hayohayo yakifanywa na CCM yaonekane hayafai na kutajwa kuwa ni ya hovyo. CCM ya JPM siyo ile ya 2015 kurudi nyuma kidogo. Hii ni tofauti na ninaiunga mkono.

Hivyo basi leo Tarehe 21/11/2016 ninatangaza rasmi kwamba ninajiunga na timu JPM kwa maslahi ya taifa kwa kuwa sioni sababu ya kupingana na yale niliyoyapigania na itakuwa ni sawa na mtu kupigana na kivuli chake mwenyewe. Kwaherini Upinzani nimeamua kuanza siasa mpya za masuala yale niliyoyaamini na ninayoyaamini. Imani ni Matendo Na Matendo ni imani. Piga vita ufisadi kwa imani na Matendo.

Moses Joseph Machali
X-mbunge, Kasulu Mjini 2010-2015,


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

Saturday, 19 November 2016

DOWNLOAD WIMBO WA MARTHA MWAIPAJA & BEATRICE MWAIPAJA UNAOITWA "HIVI NILIVYO".

DOWNLOAD WIMBO WA MARTHA MWAIPAJA & BEATRICE MWAIPAJA- HIVI NILIVYO.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

DOWNLOAD WIMBO WA ROSE MUHANDO UNAOITWA "HALLOW".

DOWNLOAD WIMBO WA ROSE MUHANDO HALLOW.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

DOWNLOAD WIMBO WA BEATRICE MWAIPAJA UNAOITWA "KUMBE NI KWA NEEMA TU".

DOWNLOAD WIMBO WA BEATRICE MWAIPAJA KUMBE NI KWA NEEMA TU .



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

Download wimbo wa Boni Mwaitege unaoitwa "Safari bado".

Download wimbo wa Boni Mwaitege unaoitwa "Safari bado".



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

#MICHEZO>>>Manchester United yabanwa mbavu na Arsenal kwenye uwanja wa nyumbani Old Trafford baada kuku bali sale ya Manchester United 1 - 1 Arsenal.Fahamu zaidi hapa.

Beki wa Man United, Antonio Valencia akipambana na wa Arsenal Nacho Monreal. Valencia alianguka na Man United walikuwa wakidai kuwa ni mkwaju wa penalti, lakini mwamuzi akasema, kipute kiendelee.




Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

#YALIYOJIRI>>>>Alichokizungumza Ester Bulaya Baada ya Mahakama Kuu Kumpa Ushindi dhidi ya Wasira.Fahamu zaidi hapa.

November 19, 2016 Kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge wa Ester Bulaya iliyofunguliwa na wapiga kura wa jimbo la Bunda dhidi ya aliyekua mgombea wa CCM Stephen Wasira ilitolewa hukumu yake ambapo Mahakamu Kuu ilimpa ushindi na kumthibitisha Ester Bulaya kuwa Mbunge halali.

Mshindi wa Ubunge wa jimbo hilo Ester Bulaya amezungumza kuelezea jinsi alivyoyapokea maamuzi ya Mahakama Kuu chini ya Jaji Noel Chocha juu ya kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na wapiga kura wanne wa mgombea Stephen Wasira.


“Kiukweli namshukuru sana Mungu, na wananchi wa jimbo la Bunda Mjini kwasababu walishaamua na mahakama imeamua lakini kwa uvumilivu wao na hivi ninavyozungumza kuna watu wametoka Musoma kwa miguu mpaka Bunda wakishangilia ushindi wa Mbunge wao” – Ester Bullaya


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

#YALIYOJIRI>>>Godbless Lema ni Shujaa wa Siasa Tanzania Asiyepigia Goti Watawala.Fahamu zaidi hapa.

Kwako Comrade G.Lema; Najua mapito unayopitia kwasasa, ni mapito makubwa sana yenye historia kubwa inayochochea hasira na kuamsha hisia Kali.

Nataka ujue na dunia ijue upo Mahabusu siyo kwasababu ya kubaka ama kuzini, upo kwasababu umekataa uonevu,umekataa kuishi ukiwa umepiga goti umekataa kuwatukuza wasiyositahili kutukuzwa, umekataa kuwapa utukufu usiyokuwa wao wala ukuu usiyositahili kwao.

Furaha yangu nipale ninapowaona wanajaribu kutisha mtu asiyeogopa mtu ambaye wakati wote amekuwa akiyaishi Yale anayonena...

Comrade Lema... najua jambo lililopo mbele yako ni jambo dogo kwako kwa aina ya siasa zako naona wanazidi kuiambia dunia na ulimwengu aina ya kamanda wanaopambana naye...

Comrade Lema... Wewe ni shujaa wetu na itabaki kuwa hivyo, unatupa somo sisi Wanasiasa wengine namna ya kuitafuta haki bila kuipigia goti, unatupa somo kubwa sana, kama tulifikiri tumefika tusahau na tuone ndiyo kwanza tumeanza Safari ya mabadiliko, Umetuamsha ya kwamba tulikuwa tumejisahau kuna wajibu tumeupuuza kipindi Fulani...

Comrade Lema.... Jina lako lipo juu ya Mlima mrefu hakuna wakufikia kileleni pale isipokuwa Jah pekee ndiyo mwenye Mkono huwo, Maono yako ni makubwa si Rahisi Mwanadamu asiye kuwa na Imani kufikiri kuwa ni imani na imani hukaa na mwenye imani...

Comrade Lema... Mara nyingi sana umekuwa ukituambia USIOGOPE nasi twasema USIOGOPE imani yetu IPO kwako...

Comrade Lema... Umekuwa ukisema ni heri ya vita inayitafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu, ni maneno ya kijasiri yanayoweza kutamkwa na mtu mwenye hofu ya mungu kwakuwa anajua alitendalo...

Comrade Lema... Huna mfano wa kufananishwa kwasasa kwa aina ya siasa zako za level ya juu sana, pengine ni kwasababu unaongoza jimbo lenye Wananchi wenye uelewa mkubwa sana, ndiyo maana umekuwa ukifikiri makubwa wakati wote.

Comrade Lema... Wananchi wako wa Arusha mjini wanakupenda sana kuliko mtu mwingine yoyote yule mpaka imefikia mahali wanazuia wasije mahakamani siku ya kesi zako, Ila hakimu ameliona hilo na kukemea, huu ni upendo wa wazi kutoka kwa Wananchi wako Mpaka walikuweka ndani Wanaona wivu wanaamua kutumia nguvu kuwazuia...wanatamani wangependwa wao Ila haitawezekana kwakuwa Wanawaarusha wanakuamini wewe...

Comrade Lema: kwasasa kila Mwanasiasa kijana anatamani kufanya siasa kama zako, huu ni utukufu usiyolazimishwa bali umekuja wenyewe kwa upendo...

Comrade Lema... Uimara wako,ujasiri wako unazidi kutuimarisha na kutupa nguvu na sababu za msingi za kutokukata tamaa, Watu wanasema, kama Mbunge anaswekwa ndani kwanini Mimi Mwananchi wa kawaida niogope kwenda ndani kama sababu ya msingi ni kukataa uonevu au dhuluma...

Comrade Lema... Kukaa kwako ndani kumewatoa watu wengi hofu ya kutokukata tamaa ya kupigania mageuzi kwakuwa huko nako wanaishi binadamu wala siyo wanyama...

Comrade Lema.... Nakutakia ijumaa njema tutakutana jumanne Mahakamani nikiwa na makamanda wengi kutoka kila pembezoni ..... Ur Comrade Henry Kilewo
NEVER SAY NEVER


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

Friday, 18 November 2016

Download wimbo mpya wa Suma Mnazaleti ft Barakah the Prince unaoitwa "Ndele".

Download wimbo wa Suma Mnazaleti ft Barakah the Prince unaoitwa "Ndele".



Download  Applicati on ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

Download wimbo mpya wa Timbulo Ft Baraka Da Prince unaoitwa "Usisahau".

Download wimbo wa Timbulo Ft Baraka Da Prince - Usisahau.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

#MICHEZO>>>VILABU VYA TANZANIA KWENYE VIWANGO VYA SOKA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa viwango vya ubora wa vilabu barani Africa ambapo timu za Tanzania zimeendelea kutokuwa kwenye namba nzuri zaidi ambapo Yanga inayoongoza kwa timu za Tanzania imeshika nafasi ya 331.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania  Yanga SC imeshika nafasi ya 331 huku Azam FC ikishika nafasi ya 351na Simba ikiwa nafasi ya 356.

Yanga wamepata pointi nyingi kutokana na ushiriki wao katika michuano ya CAF wakivuka raundi ya pili klabu bingwa Afrika msimu wa 2015-16 na kufika hatua ya nane bora kombe la Shirikisho.

Etoile du Sahel ya Tunisia ndio inaongoza ikifuatiwa na TP Mazembe ya DR Congo huku Esperance de Tunis ikishika nafasi ya nne mbele ya Vita Club ya DR Congo na Al-Merreikh ya Sudan ikifunga tano bora.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

Mwanaume Fanya Hivi ili Mkeo Akuone Mtenda Miujiza Kila Siku..Hakika Hatasikia la Mtu.Fahamu zaidi hapa.

Hili ni fundisho kwa vijana wengi ambao wanataabika, suala la fedha limekuwa mwiba mkubwa na chanzo kikubwa cha mahusiano na ndoa kuyumba. Nimelazimika nije na ushauri huu ambao utawasaidia vijana wa kileo ambao wanataabika na ndoa hususani suala la fedha.

Kinachowaumiza vijana wengi katika fedha na wenza wao ni tabia ya wanaume kuwa wazi kwa kutoa taarifa za pato lake kamili. Jambo la uwazi ni jema lakini muwe na kiasi kwani usipokuwa na akiba ya 'taarifa za kipato chako' utakosa fusra ya kufanya miujiza pale mambo yanapokwama.

Fanya hivi. Mfano kipato chako ni shilingi milioni moja kwa mwezi, mweleze kwamba unapokea shilingi laki 7 na hizo tatu hakikisha unaweka katika sehemu salama ambayo hata ikitokea umekufa familia yako itafaidika, mfano benki kila unapochukua mshahara hakikisha unaacha laki tatu kama akiba asiyoijua. Sasa katika hii laki saba panga matumizi pamoja na akiba ya pamoja.

Wanawake wanapenda 'mshtuko/suprise'..so siku ya siku ukiona kanuna unamtoa shoping lazima ataona umetenda muujiza kwa nia njema. Hapa ndipo pale utasikia mwanamke anasema 'mme wangu ana akili kweli'. Ikitokea una marupurupu fulani kama safari nk hakikisha unatoa kiasi na ziada unaweka chimbo. Hii itakupa upenyo wa kuwasaidia hata wazazi wako na ndugu zako bila kumhusisha mara kwa mara kwani wanawake wengine hawapendi usaidie ndugu na jamaa. Fanya mbinu hii hata kama kipato chako ni laki tano weka hata elfu hamsini chimbo ili uweze kutenda baadhi ya miujiza.

Wanawake wote duniani wamejaliwa karama ya kutumia hela yote ya mmewe, yaani ukimwambia kuna hela hii yeye ataandika orodha ya mahitaji ya familia ni kwani njema ila pesa zikiisha yeye hujitoa na kukulaumu kwanini ulitumia pesa zote. Yaani dharura ikitokea yeye hayupo ni lako hilo na ukishindwa kutatua hapo ndipo dharau inaanza...utasikia 'mme wangu hana msaada kabisa' yaani hajali kabisa matatizo anatumia pesa zote bila uangalifu.

Haya yote yanahitaji ustadi mkubwa na utimamu, kumbuka siku zote mwanaume anatakiwa kuwa mtu wa mshitukizo/surprise kwa kutumia kipato kile kile alichonacho. Yaani tunasema uwe na uwezo wa kutengeneza hela (money creator). Ikitokea dharura unamuangalia usoni huku ukitabasamu, unamwambia 'mke wangu usihuzunike ngoja nifanye mpango nitatue hii shida'.

Hii ndio mbinu tuliitumia sisi na kuweza kuishi na mama/bibi zenu bila bugdha.

Nawakilisha.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

#MICHEZO>>>Simba yafunguka kuhusuujio wa Emmanuel Okwi na Kipre Tchetche.Fahamu zaidi hapa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu ya Simba Zacharia Hanspoppe amekanusha usajili wa washambuliaji Emmanuel Okwi na Kipre Herman Tchetche ndani ya klabu hiyo katika dirisha dogo la usajili.
Emmanuel Okwi na Kipre Tchetche.
Amesema habari zinazosambaa kuhusu usajili wa wachezaji hao siyo za kweli kwani kamati inakutana hii leo kwa ajili ya kupitia ripoti ya kocha na mara baada ya kikao hicho ndipo wataangalia mapendekezo ya kocha kuhusu usajili kwani mpaka sasa bado hawajafanya mazungumzo na mchezaji yoyote wa ndani au nje ya nchi.

Hanspoppe amesema, mshambuliaji Emmanuel Okwi kwa sasa yupo nchini Denmark na hakuna kiongozi ambaye ameshaenda kufanya mazungumzo naye kuhusu usajili, na kwa upande wa Kipre pia hawajawahi kufanya mazungumzo.
Zacharia Hanspoppe

Wakati huohuo Hans amesema, ndani ya klabu ya Simba hakuna mchezaji ambaye yupo katika mazungumzo na klabu yoyote kwani wachezaji hao wote wana mikataba ambayo inawafanya kuwa ni wachezaji halali wa Klabu hiyo.

Amesema, wachezaji  walio ndani ya klabu hiyo mikataba yao inaisha Juni 15 mwakani na wana uamuzi wa kuongea nao muda wowote na hata usajili unafanyika mara baada ya kumalizika kwa mkataba.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

#YALIYOJIRI>>>>Mamlaka ya Bandari Bandari yapokea boti mbili za kuegesha meli.Fahamu zaidi hapa.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepokea boti mbili za kisasa za kuhudumia meli kutoka China zitakazotumika katika Bandari za Dar es Salaam na Tanga.
 Meneja Mawasiliano wa TPA, Janeth Ruzangi alisema ujio wa boti hizo zilizopolewa jana utasaidia kuongeza kasi ya utendaji kazi na ufanisi katika bandari hizo. 
Alisema ujio wa boti hizo ni sehemu ya mkakati wa TPA kuongeza vitendea kazi kwa upande wa majini na nchi kavu ili kuongeza kasi ya upakuaji na upakiaji wa mizigo kwa kiwango cha kimataifa na hivyo kuvutia wateja wengi. 
Nahodha Mkuu wa TPA, Kapteni Abdullah Mwingamno alisema boti ya tani 70 iliyopewa jina la Valeria Rugaihuruza itabaki Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudumia meli zinazoshusha mafuta katika Boya la SPM lililopo Mji Mwema, wakati nyingine inayoitwa Mwambani itapelekwa Bandari ya Tanga kwa ajili ya kuhudumia matishari. 
Boti ya MV Valeria Rugaihuruza imeundwa na ‘crane’ yake pamoja na boti nyingine ndogo mbili ndani yake kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi kwenye boya la mafuta. Boti ya MV Mwambani ina uwezo wa kuvuta tishari lenye uwezo wa kubeba tani 3,500 za mizigo.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

#BURUDANI>>>>Mimba ya Nisha Bebee Yazua Balaa..Adai Baba Kijacho Wake Hawezi Hata Kujinunulia Sabuni ya Kufulia Boxer.Fahamu zaidi hapa.

Ujauzito wa Mwigizaji Nisha Bebee umezidi kuzua sinto fahamu kutokana na vichambo anavyopost mtandaoni kwenda kwa Muhusika wa Ujauzito huo..leo tena amepost akimtolea uvivu kama ifuatavyo:
"Watu wanasema nimepewa mimba na kutelekezwa, guyz kuna tofauti kati ya kutelekezwa na kutotaka mtoto wako amjue baba ake.
 
Since nimeamua kuwa wazi wananipigia kama machizi.. NASEMA HIVI SUBIRINI DNA ZA MACHO naanzaje kumtambulisha mwanangu kwa baba namnunulia hadi sabuni ya kufulia boxer mwanaume mzima unaolewa na demu.. star ushuzi star jina pesa hana mfukoni tena koma kutuma marafiki zangu.. tena moods zangu za sasa hivi sizo nichokonoe nikupost unazopiga vizinga hela za maandalizi ya show xiiew.. I'M DONE" Nisha


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

 

#YALIYOJIRI>>>PAUL Makonda "Mnasubiria Nitumbuliwe, Mimi Najua Nipo Kwa Kusudi la Mungu".Fahamu zaidi hapa.

Baada ya kauli ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kusema atamwajibisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda iwapo hatasimamia ipasavyo kukomesha matumizi ya dawa za kulevya, aina ya shisha, Makonda afunguka.

Akiongea Ijumaa hii katika kipindi cha Power BreakFast kinachorushwa na Clouds FM, Mkuu huyo amesema anajua kuwa kazi za serikali ni zakupita huku akidai yeye anamtegemea Mungu katika kazi zake.

“Mimi bahati mbaya ninajua kuwa hizi kazi ni zakupita watu wengine unakuta wanasema huyu jamaa atanyooshwa tu, atatumbuliwa, tutaona mimi sikomolewi kwasababu mimi najua nipo kwa kusudi la Mungu. Wakati wa Mungu ukipita mambo mengine yatajitokeza, lakini ninachokijua ni kitu kimoja asilimia 80 ya watu hawafanyi kazi ipasavyo katika ofisi zao,”

Aidha Makonda alisema ripoti nyingi anazoletewa zinaonyesha mtaani hali ni shwari lakini akienda kuzungumza na wananchi unakuta mambo tofauti na yale yalioandikwa kwenye ripoti.

Pia mkuu huyo amezindua kampeni iitwayo ‘Dar es salaam Mpya’ ambayo itamfanya kuzunguka katika sehemu mbalimbali za jiji hilo kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzipatia majibu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE