Uongozi wa klabu ya Simba umeitisha mkutano wa wanachama wa dharura utakaofanyika Desemba 11.
Mkutano
huo umeitishwa baada ya kikao cha kamati ya utendaji wa klabu hiyo
iliyokaa juzi. Mkutano huo utafanyika kwenye Ukumbi wa Maofisa wa Polisi
Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema kamati ya utendaji imetoa baraka zake kupitia ibara ya 22 ya katiba ya Simba.
“Mkutano huo utakuwa ni mwendelezo wa mkutano wa kawaida uliofanyikaJulai 31, 2016,” alisema Manara.
Ingawa
taarifa hiyo kwa vyombo vya habari haijafungua kila kitu, lakini
inaonekana mwendelezo utakuwa ni ule kuhusiana na kuboresha suala la
uongozi Simba na kuingia katika suala la uwekezaji kama ambavyo
mfanyabiashara Mohammed Dewji alivyojitokeza.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment