Hatimaye rufaa ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema iliyokatwa na mawakili wake itasikilizwa Jumatatu ijayo.
Rufaa
hiyo itasikilizwa na Jaji Fatma Masengi ya kuomba mbunge huyo kupewa
dhamana baada ya mawakili wanaomtetea jana kusajili maombi ya rufaa
namba 112/113 ya mwaka 2016 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, ili kudai haki
ya dhamana ya Lema aliyonyimwa kutokana na makosa ya kisheria
yaliyofanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
Rufaa
hiyo imepokewa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na kupangwa kwa Jaji
Masengi ambaye ndiye atakayeamua hatma ya Lema kuwa nje kwa dhamana au
la.
Mawakili
wa Lema ambao ni Sheck Mfinanga na Peter Kibatala jana walisema tayari
wamesajili rufaa yao Mahakama Kuu na wanasubiri siku hiyo ili
isikilizwe.
Mfinanga
alisema wameamua kufungua maombi ya rufaa kwa ajili ya kujua ni kwa
nini Lema amekosa dhamana ambayo awali Hakimu Desdery Kamugisha alisema
ipo wazi.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment