Msanii mkongwe wa muziki Khalid Mohamed aka TID ameingia kwenye mgogoro na kituo cha redio cha Clouds FM baada ya kukituhumu kituo hicho kimejiingizia fedha kwa kuhadaa wao ndio waliotayarisha wimbo wa Zeze.
Muimbaji huyo ametoa tuhuma hizo kupitia mtandao wa kijamii wa istagram pamoja na kuweka kielelezo cha kava ya CD ambacho amedai amekipata nchi za nje.
Kupitia instagram, TID alipost picha (hapo juu) na kuandika:
HII NI DHULUMA YA WAZI WAZI HUU WIMBO UMEFANYIKA KWELI CLOUDS MALIPO YOTE YAMELIPWA CLOUDS….BRAZA RUGE NAOMBA HELA ZANGU hivi Clouds FM mshawahi Kutenengeneza Zeze Song. .!? I WANT MY MONEY SHOW ME CONTRACT naomba Hakuna Yangu Sikuogopi I want Clouds FM kwa Kudanganya hivi wanilipe Milioni Mia Tano ….Ushapata Pesa Nyingi Sana Hauna Haja ya kuendelea,My Legal Team is Ready to Bring this Fake Institution Down
Bongo5 ilimtafuta TID na kuzungumza naye ili kujua ukweli kuhusu taarifa hizo na atachukua hatua gani ili kuisaka haki yake.
“Ile ni CD ambayo imeuzwa Marekani na duniani kote na yale ndio maelezo yake,” alisema TID. “Hiyo kazi ipo Mahakamani, naenda Mahakamani, kwahiyo nahitaji wanasheria ambao watapigana kupata haki yangu,”
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment