Friday, 28 August 2015

#MICHEZO>>>TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE TWIGA KUFUNGUA DIMBA NA IVORY COAST.

TIMU ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inayotarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi Agosti kuelekea nchini Congo-Brazzavile kwenye Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) imepangwa kufungua dimba na timu ya Wanawake ya Ivory Coast Septemba 6, 2105.
 Twiga Stars iliyoweka kambi kisiwani Zanzibar kwa takribani mwezi mmoja sasa, itacheza mchezo wake pili Septemba 9, dhidi ya Nigeria kabla ya kumalizia mchezo wake wa mwisho hatua ya makundi dhidi ya wenyeji Congo-Brazzavile Septemba 12, 2105. Jumla ya timu nane za Wanawake kutoka Barania Afrika zinashirki fainali hizo ambazo ni Nchi za Afrika Kusini, Cameroon, Ghana, Misri (wamejitoa) kundi B, na wenyeji Congo-Brazzavile, Ivory Coast, Nigeria na Tanzania kutoka kundi A. Timu mbili za juu kutoka kila kundi zitafuzu kwa hatua ya nusu fainali.
Toa maoni yako hapa.

0 comments:

Post a Comment