Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji,
Damian Lubuva akitoa mada leo jijini Dar es salaam kwa viongozi wa madhehebu
mbalimbali waliohudhuria mkutanoni .
Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria
mkutano ulioandaliwa na NEC leo jijini Dar es salaam wakifuatilia mada
iliyokuwa zikiendelea.
Wanasekretarieti ya maandalizi ya
mkutano NEC na wadau mbalimbali na baadhi ya waandishi wakifuatilia
mjadala kuhusu wajibu wa viongozi wa dini kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya uchaguzi
Jaji, Damian Lubuva akiteta jambo na mmoja wa makamishna wa Tume hiyo
Prof Amon Chaligha leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa NEC na wadau
mbalimbali.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.
Kailima Ramadhani akitoa mada kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi na hatua
zilizofikiwa hadi sasa leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa viongozi
wa madhehebu ya dini.
MWANDISHI WETU -MAELEZO-DAR ES SALAAM
Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC
imewaomba viongozi wa dini zote kutumia majukwaa yao kuwaelimisha wapiga
kura bila kuonyesha hisia za kuegemea upande wowote wa mgombea ili waweze
kufanya maamuzi sahihi wakati wa uchaguzi Mkuuu ujao.
Kauli
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva kwenye
Mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam uliowakutanisha wadau hao wa
uchaguzi na kuwakumbusha wajibu wao katika jamii hususani katika kipindi hiki
ambacho nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.
Alisema kuwa taasisi za kidini zinaaswa
kama walivyo wadau wengine katika kipindi hiki cha uchaguzi kuhubiri amani na
kuendelea kutoa elimu kwa watanzania ili zoezi hili liishe kwa amani na
kuwaacha watanzania wakiwa na umoja na mshikamano licha ya tofauti za
kiimani zilizopo miongoni mwao.
“Tume inawataka, nyinyi viongozi wa
dini, mnapotoa mafundisho ya uchaguzi kwa waumini wenu kuhakikisha hamuonyeshi
hisia za kuwa upande wa chama chochote cha kisiasa na zaidi kuepuka kushawishi
waumini wenu kuegema chama au mgombea fulani” amesema Jaji Lubuva.
Mmoja
wa washiriki wa mkutano huo , Askofu Philemon Phiri wa kanisa la EAGT-Mikocheni
-A ameiasa Tume hiyo kusimama katika haki, uhuru na kuhakikisha
wanatangaza washindi bila kuonyesha upendeleo ili kuivusha nchi ikiwa
salama.
Mshiriki mwingine kutoka Kanisa la Moravian
Mchungaji Alamu Kajuna alisema kuwa amani ndiyo tunu kwa kila mwanadamu,
hatutegemei vurugu wakati huu wa uchaguzi maana amani inapotoweka
wanaoumia ni wananchi wakiwamo waumini wao hivyo wao kama taasisi
zinazoshirikiana na wananchi kwa karibu kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi
ili tupate viongozi kwa Amani.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekutano na
viongozi hao na wadau wengine ikiwa zimebaki siku mbili kuanza kwa kampeni hapo
Jumamosi ijayo kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao.
Chanzo
Michuzi.
0 comments:
Post a Comment