Meli kubwa kabisa kuwahi kuingia katika bandari ya Dar es Salaam, Clemens Schulte. Meli hiyo yenye urefu wa mita 255 ilitia nanga nchini 26 Agosti 2015 na kufunga gati katika kitengo cha Kontena kinachoendeshwa na Kampuni binafsi ya TICTS katika bandari ya Dar es salaam siku iliyofuata.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bi. Apolonia Mosha (katikati) akiwa na nahodha Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Capt. Abdul Mwingamno (kulia) na Kaimu Meneja Mawasiliano wa mamlaka hiyo, Bi. Janeth Ruzangi wakati wa tukio la kukaribisha kuwasili kwa meli kubwa kuwahi kufika katika bandari ya Dar es Salaam. Meli hiyo, MV. Clemens Schulte, yenye urefu wa mita 255 ilitia nanga nchini 26 Agosti 2015 na kufunga gati katika kitengo cha Kontena kinachoendeshwa na Kampuni binafsi ya TICTS katika bandari ya Dar es salaam siku iliyofuata.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Makasha (TICTS), Bw. Paul Wallace (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Maendeleo wa kampuni hiyo, Bw. Donald Talawa (kushoto) wakimsikiliza nahodha Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Capt. Abdul Mwingamno (kulia) wakati wa tukio la kukaribisha kuwasili kwa meli kubwa kuwahi kufika katika bandari ya Dar es Salaam. Meli hiyo, MV. Clemens Schulte, yenye urefu wa mita 255 ilitia nanga nchini 26 Agosti 2015 na kufunga gati katika kitengo cha Kontena kinachoendeshwa na Kampuni binafsi ya TICTS katika bandari ya Dar es salaam siku iliyofuata
Uongozi wa kitengo cha kimataifa cha makasha (TICTS) umepongeza juhudi zinazoendelezwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) za kuimarisha bandari ya Dar es Salaam.
Akiongea wakati wa kukaribisha kuwasili kwa meli kubwa kabisa kuwahi kufika katika bandari hiyo, Afisa Mkuu Mtendaji (CEO) wa TICTS, Bw. Bw. Paul Wallace aliuita ujio huo kuwa wa muhimu sana kwa maendeleo ya bandari hapa nchini.
“Tunaona maendeleo makubwa ya kiutendaji katika bandari yanayopelekea mashirika makubwa kama Maersk Line kuleta meli zake katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki,” alisema mwishoni mwa wiki.
Alisema ujio wa meli hiyo pia ni uthibitisho wa ushirikiano wa wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuwa bandari ya Dar es Salaam inafunguka zaidi kimataifa.
Meli hiyo yenye urefu wa mita 255 ilitia nanga nchini 26 Agosti 2015 na kufunga gati katika kitengo cha Kontena kinachoendeshwa na Kampuni binafsi ya TICTS katika bandari ya Dar es salaam siku iliyofuata. Meli hiyo iliyoongozwa na nahodha Vladislav Barisovscy inajulikana kama Clemens Schulte ina uwezo wa kubeba makontena 5466.
Wakati wa safari hiyo ya kwanza, MV. Clemens Schulte yenye ukubwa wa Postmanax ilishusha makontena 250 na kupakia mengine 1300. Bandari ya Dar es Salaam iko katika mageuzi makubwa kuifanya ya kisasa zaidi ambapo moja ya maboresho yaliyofanyika hvi karibuni ni pamoja na kuanzisha mfumo wa malipo ya huduma za bandari kwa njia ya kielektroniki na kufunga mifumo mipya ya kisasa ya ulinzi ikiwa ni pamoja na CCTV. “Tunajivunia bandari yetu, tumeongeza ufanisi na tuko tayari kupanua zaidi huduma zetu,” alisema.
Bw. Wallace alisema TICTS iko katika harakati za kununua mashine kubwa zaidi za kubebea mizigo zenye thamani ya Tshs bilioni 46 zitakazowezesha kampuni hiyo kuhudumia meli kubwa zaidi ya Clemens Schutle na hivyo kuifanya bandari ya Dar kuwa shindani katika ulimwengu unaobadilika kwa kasi.
Kaimu Meneja Mawasiliano wa TPA, Bi. Janeth Ruzangi alisema ujio wa meli hiyo toka bandari ya Laem Chabang ya nchini Thailand ni uthibitisho wa kuzidi kuaminika kwa bandari hiyo kimataifa.
“Uaminifu huu unatokana na kuimarika kwa huduma tunazotoa,” alisema. Mkurugenzi wa Maendeleo TICTS, Bw. Donald Talawa alisema ujio wa meli hiyo ni kielelezo cha ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi ambao unatakiwa kuigwa na wadau wengine nchini.
Mara ya mwisho Kitengo hicho kupokea meli kubwa ilikuwa mwezi Februari 2014 ambapo meli iliyoitwa Msc Martina iliyokuwa na urefu wa mita 242. Pamoja na kuhudumia wateja wa ndani bandari ya Dar es Salaam pia inahudumia nchi za DRC Congo, Zambia, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi na Zimbabwe.
0 comments:
Post a Comment