Wanariadha Mo Farah wa Uingereza na Usain Bolt wa Jamaica wameendelea
kuitikisa dunia kwenye mchezo huo, baada ya kutwaa medali nyingine za
dhahabu.
Wakati Farah, mzaliwa wa Somalia aliyekimbilia Uingereza kukwepa
machafuko akizoa medali ya dhahabu kw akukimbia umbali wa mita 5,000 kwa
Dakika 13:50.38, Bolt alipata dhahabu ya 11 baada ya kushinda kwenye
mbio za kupokezana vijiti kwa watu wanne umbali wa mita 100.
Huu ni ushindi wa tatu mfululizo kwa Farah aliyepata pia kutwaa dhahabu
kwenye mashindano ya dunia lakini pia kabla kwenye michuano ya Olimpiki.
Haikuwa ushindi rahisi kwa Farah, wala hakuongoza muda wote wa mchezo,
kwani mshindi wa Kenya kwenye michuano ya Jumuiya ya Madola, Caleb Ndiku
aliongoza kwa kipindi fulani.
Hata hivyo, Farah aliongeza kasi na kumpita Ndiku kwenye kona ya mwisho
na kujihakikishia medali ya saba ya dhahabu ya dunia. Alieleza furaha
yake kwa kutwaa ubingwa lakini zaidi kuweka historia duniani.
Alidokeza kwamba hakuwa anajihisi timamu sana kiafya, kwani misuli ya
paja ilionekana kutaka kumharibia mambo lakini jopo la madaktari wake
wakamsaidia. Akasema kwamba awali alihisi woga lakini hatimaye mambo
yakaenda vyema.
Kwa upande wa Bolt, alifanya vyema na wenzake watatu walipopokezana
vijiti na kumaliza mita 100 kwa sekunde 37.36, na kwa Bolt ilikuwa
ukamilisho wa dhahabu tatu katika mashindano haya, kwani alitwaa ya
kwanza kwenye mbio za mita 100 na kisha mita 200.
Toa maoni yako hapa.
0 comments:
Post a Comment