HOTUBA YA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA
CHA CHADEMA NA UKAWA MH. EDWARD NGOYAI
LOWASSA
YA KUZINDUA ILANI NA KAMPENI YA UCHAGUZI
MKUU
Jangwani-Dar-es-Salaam, 29 AGOSTI 2015
Ndugu Wana Dar es salaam na Watanzania
wenzangu
1. Leo ni siku ya kihistoria. Baada ya miaka ishirini
na tano tangu mfumo wa vyama vingi urejeshwe,
vyama vya upinzani wa CHADEMA, CUF, NCCR na
NLD umeungana chini ya Umoja wa Katiba ya
Wananchi kupigania uchaguzi mkuu wa mwaka huu
na kuwa na mgombea mmoja katika ngazi zote.
2. Miaka zaidi ya hamsini ya utawala wa serikali za
CCM na waasisi wake, umekuwa utawala wa
wachache walio hodhi madaraka na mali za nchi.
3. Leo tunaanza safari ya uhakika ya kuleta
mabadiliko ya kweli nchini.
a. Mabadiliko yaletayo neema na kujenga upya
mfumo wa uchumi, haki na sheria nchini.
b. Mabadiliko ya kuimarisha huduma za jamii kama
elimu, afya, maji na makazi.
c. Mabadiliko ya kuondoa umaskini.
d. Mabadiliko tunayatoahidi ni mabadiliko ya
kurejesha matumaini kwa Watanzania kwa kubadili
hali zao za maisha.
4. Kila mwaka hali na ubora wa maisha ya
Watanzania imeshuka wakati tunaambiwa kuwa
pato laTaifa linakuwa.
5. Lakini Watanzania wanachotaka siyo takwimu
bali kuona kipato chao kinakua, shule, hospitali na
barabara bora zinajengwa.
6. Wanataka kupata maji safi na salama ya kunywa.
Wanataka makazi bora.
7. CHADEMA na UKAWA, tuna dhamira ya kuleta
mabadiliko ya kweli ili kuona azma ya Watanzania
tangu uhuru ya kuondoa umaskini, maradhi,na
ujinga inahitimishwa.
8. Ili tufanye hivyo tuahitaji tufanye mabadiliko ya
fikra, uongozi, sera na utendaji.
9. Leo Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi
za ki-uchumi, kisiasa na kijamii. Changamoto hizi ni
matokeo ya sera za utawala wa Chama kimoja wa
miaka hamsini. Sote ni wahanga wa siasa na sera
hizi.
10. Miaka Hamsini ya CCM imetosha. Tunataka
mabadiliko na siyo ahadi zile zile kila mwaka.
11. Tusidanganyike, CCM hawana jipya.
12. Chagueni UKAWA wenye dira ya kubadili maisha
ya wananchi.
13. Mimi ninauchukia umaskini na mimesimamia
maendeleo kwa vitendo. Nilipokuwa Waziri Mkuu
nilijaribu kubadili hali hii. Nilisimamia ujenzi wa
shule za kata, Chuo Kikuu cha Dodoma.
Nilihakikisha mikataba mibovu ya maji inavunjwa na
sasa wananchi wa kanda ya ziwa wanapata maji
safi.
Ndugu watanzania
14. CCM wanauliza tuna mpango gani wa kumaliza
umaskini. Sisi hatuahidi tu. Tutatenda.
15. Ilani yetu ni dira ya kuondoa umaskini kwa
mikakati sahihi na siyo nadharia.
16. Mkakati wa kuondoa umaskini si wa sekta kwa
sekta bali wa sekta zote kwa pamoja. Ni ujumla wa
utendaji na utekelezaji wa sera za kila sekta utakao
leta maendeleo.
17. Mkakati wangu na UKAWA wa kuondoa
umaskini utakuwa na nguzo tano:-
a. Kupunguza matumizi ya serikali na mashirika
yake na kuimarisha utendaji na uwajibikaji.
b. Kukuza pato la serikali kwa kudhibiti ukwepaji na
misamaha ya kodi holela na kuhakikisha nchi
inawekeza katika sekta muhimu na inapata gawio
halisia kutoka wawekezaji
c. Kukuza uchumi kwa sera na sheria endelevu
ikiwa ni pamoja na kukuza biashara na uwekezaji
hasa katika sekta za madini, kilimo, viwanda, ufugaji
na uvuvi na kuondoa kodi kwa wanyonge.
d. Kuimarisha huduma za umma kama elimu, afya,
maji na makazi, na mazingira
e. Kuimarisha utawala bora na mfumo wa haki na
sheria chini ya Katiba ya Wananchi.
18. Chini ya misingi hii na ili kufanikisha mkakati wa
kuondoa umaskini, serikali yangu itafanya
yafuatayo:-
ELIMU BORA KWA KILA MTANZANIA
Nimelisema hili huko nyuma. Nalisema tena leo.
Elimu kwanza, Elimu kwanza, Elimu kwanza.
Kwa hiyo mkakati wetu wa msingi utakuwa kutoa
Elimu itatayogharamiwa na serikali kwa kila
Mtanzania kutoka elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu
na pia:-
1. Kuimarisha elimu ya teknolojia, ustadi na ufundi
inayojenga uwezo wa kujiajiri na ushindani katika
soko la ajira.
2. Ujenzi na uimarishaji wa miundombinu ya elimu
ikiwa ni pamoja na shule za Kata.
3. Kusimamia ubora wa viwango vya elimu kote
nchini.
4. Kuimarisha taaluma na mitaala katika mashule.
5. Kuondoa utoro darasani, na kuboresha afya za
wanafunzi.
6. Kuboresha maslahi na vitendea kazi kwa walimu
ikiwa ni pamoja na nyumba, posho ya kufundishia,
usafiri na zana za teknolojia.
7. Kufuta michango ya maabara ya shule za kata
AFYA
1. Afya na tiba ya kila Mtanzania itagharamiwa
kupitia bima za gharama nafuu na mifuko ya hifadhi
ya jamii
2. Tutaimarisha afya ya msingi pamoja na kinga
kupunguza gharama za tiba.
3. Serikali itahakikisha kuna uwiano na upatikanaji
wa watumishi wa afya katika kada mbalimbali ili
kuleta tija na huduma stahiki.
4. Itaimarisha miundombinu ya afya pamoja na
kujenga hospitali za kisasa ili kusogeza huduma za
afya karibu na jamii na pia kuepukana na tiba za nje
ya nchi.
5. Tutarejea kwa lengo la kuboresha maslahi na
vitendea kazi katika sekta ya Afya ikiwa ni pamoja
na nyumba na usafiri.
6. Tutathibiti ongezeko la gharama za huduma za
afya bila kuathiri uendeshaji wa watoaji huduma za
afya kama vile serikali na hospitali za sekta binafsi.
ARDHI, MAJI NA KILIMO
1. Tutaimarisha mfumo wa umiliki wa ardhi kwa
0 comments:
Post a Comment