Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa,
Balozi Celestine Mushy (kushoto) kwa pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakichanganya saruji, kokoto na mchanga
ili kupata zege kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi ikiwa ni uzinduzi
wa kuanza kwa ujenzi wa vyoo 22 kwenye Shule ya Msingi Kiboriloni, Mkoani
Kilimanjaro. Uzinduzi huo ni tukio mojawapo kuelekea maadhimisho ya miaka 70 ya
kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa Ujenzi huo umedhaminiwa na
UNDP.
Mwakilishi wa UNFPA Dkt. Nathalia Kanem naye
akimpatia fundi tofali la ujenzi wa vyoo hive
Balozi Mushy naye akiweka tofali katika
msingi huo
Bw. Alvaro akiweka jiwe la msingi
kuzindua kuanza kwa ujenzi wa Vyoo hivyo
0 comments:
Post a Comment