Sunday, 30 August 2015

Tukumbushane watu wangu Sheria ya Mitandaoni.Sheria ipo hapa.

Sheria ya mitandao inaanza kutumika rasmi tarehe 1 September 2015, haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia ili kuepukana na mkono wa dola: 1. Tujiepushe kusambaza ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii kupitia mitandao; 2. Tujiepushe kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta uchochezi wa kidini unaoweza kupelekea kuvuruga Amani na maelewano kwa jamii kupitia mitandao; 3. Tujiepushe kusambaza picha ama video za utupu ama zilizokosa maadili kwa jamii kupitia mitandao; 4. Tujiepushe kusambaza picha ama video za uchochezi wa kidini ama kisiasa kupitia makundi mbalimbali ama mitandao ya kijamii; 5. Tujiepushe kusambaza kwa wengine ujumbe wowote unaohusiana na mambo yaliyotajwa 1 – 4; 6. Tujiepusha na kufanya wizi kupitia mitandao mbalimbali ya simu; 7. Tujiepushe kumpatia mtu yeyote line zetu za simu ili zitumike kufanya wizi au utapeli wa mitandao ya simu; 8. Tujiepushe kushiriki kumchafua mtu, taasisi, kikundi cha watu kwa namna yoyote kupitia mitandao; 9. Tujiepushe na tabia ya kutokutoa taarifa polisi juu ya upotevu wa simu au kifaa chochote cha kielektroniki kinachoweza kutumika kwa mawasiliano ya kimtandao; 10. Tujiepushe kutumia mtandao kwa utapeli kupitia “brand” ama jina la mtu; 11. Tujiepushe na “ujamaa” wa kushirikiana vifaa vya kielektronic na mtu yeyote yule hata kama unamuamini sana; 12. Tujiepushe na kumtajia mtu password zetu au email account zetu kwa namna yoyote ile (kila mtu au mwanafunzi aliyeko field atumie username na password yake akitaka kutumia computer za company); 13. Tuhakikishe kwamba website yoyote inayotuhitaji kutumia username na password zetu ipo secured. Website zote zilizo secured address (url) huanzia na https://; 14. Tukumbuke kutoa elimu hii kwa watoto, ndugu, marafiki na majirani zetu.
Toa maoni yako hapa.

0 comments:

Post a Comment