Hatimaye Mario Balotelli anaelekea kuondoka Liverpool kurudi nyumbani
kujaribu maisha AC Milan kwa mkopo wa msimu mzima, baada ya kuvurunda
msimu uliopita Anfield.
Mshambuliaji huyo wa kati
alikamilisha vipimo vya afya Milan, ambapo atapunguziwa malipo yake
kiasi, huku Liverpool wakiendelea kulipa sehemu ya mshahara wake akiwa
Italia. Huenda atacheza mechi ya Jumamosi dhidi ya mahasimu wa Milan,
Empoli.
“Milan wamekuwa daima moyoni mwangu na nilikuwa na
matumaini kwamba siku moja ningerudi hapa. Je, nitamalizia maisha yangu
ya soka hapa? Hilo litakuja baadaye, natakiwa kufanya kazi kwa bidii
ili niwe na mwaka mzuri.
“ Nasubiri kwa hamu kuanza
mazoezi na kuonesha watu kwamba nina thamani. Nina motisha nyingi za
kufanya vizuri lakini naomba nianze kufanya kazi na si kuongea,” akasema
Mtaliano huyo mtata mwenye umri wa miaka 25.
Balotelli
akiwa ndiye tegemeo la Liverpool msimu uliopita alifunga bao moja tu
kwenye ligi kuu nchini England, baada ya kuwa amesajiliwa kwa pauni
milioni 16 kutoka Milan Agosti mwaka jana.
Hakuambatana na
timu kwenye ziara ya kabla ya msimu Mashariki ya Mbali na Australia na
amekuwa akifanya mazoezi nje ya kikosi cha kwanza.
Alikuwa
anaonesha hapendi kuondoka Liverpool kutokana na malipo mazuri licha ya
kocha Brendan Rodgers kujenga mazingira ya kumwondoa, lakini baada ya
kusajiliwa kwa washambuliaji wakali, Christian Benteke, Roberto Firmino
naDanny Ings, huku Divock Origi akirejea Anfield kutoka Lille alikokuwa
kwa mkopo, Balotelli ameona hana namba kabisa.
0 comments:
Post a Comment