Zaidi ya wanachama 500 wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiwemo viongozi wa kata mbalimbali
katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, wamekihama chama hicho na kujiunga na
chama cha ACT-Wazalendo.
Wanachama hao wamefikia maamuzi
ya kukihama chama hicho huku wakiwalalamikia viongozi wao wa CHADEMA wilaya na
taifa kumkata mgombea wao wa ubunge jimbo la Ludewa waliyemuhitaji Bwana Okol
Haule na kumuweka mgombea wanayemuhitaji wao bwana Bathoromeo Mkinga.
Mamia ya wanachama hawa kutoka
wilaya ya Ludewa, wamefanya maandamano ya amani kutoka mtaa wa Kilimahewa hadi
katika ofisi za chama hicho zilizopo mjini Ludewa wakiwa na mabango ya aina
mbalimbali yakilaani viongozi wa CHADEMA wilaya na taifa kumkata Okol Haule
aliyeshinda katika kura za maoni kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.
Hata mara baada ya wanachama hawa
kuwasili katika ofisi za CHADEMA wilaya, viongozi waliingia mitini na kufunga
ofisi, lakini dhamira ya wafuasi hawa wa CHADEMA wakiwemo viongozi wa juu
kutoka kata mbalimbali za wilaya ya Ludewa, haikuishia hapo na wote wakiwa
hawana imani tena na CHADEMA wakaelekea ofisi za ACT Wazalendo mtaa wa Sokoni
na kujiunga nacho.
Huku wakidhamiria kuisambaratisha
kabisa CHADEMA wilayani humo, wanachama hao wakiungana na mgombea wao
wanayemuhitaji bwana Okol Haule wakachoma moto nguo aina ya kombati alizokua
akizitumia mgombea huyo, bendera na kadi za CHADEMA ambapo bwana Haule anasema
ameshindwa kuvumilia ubakaji wa demokrasia uliofanywa na viongozi wa CHADEMA.
0 comments:
Post a Comment