Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na watoto Mhe. Dkt. Pindi H. Chana (Mb)akimpongeza Bi. Jane Malyi
kiongozi wa wahitimu wa mafunzo ya ujasiriamali na urembo mara baada ya kutoa
neno fupi kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo katika chuo Kikuu Huria cha
Tanzania, jijini Dar es salaam
Na erasto Ching’oro Wasichana 22 kutoka
mazingira hatarishi wamehitimu mafunzo ya ujasiriamali, mawasiliano, ususi wa
nywele na urembo katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania jijini Dar es salaam na
kutunukiwa vyeti vya umahiri na Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia na watoto Mhe. Dkt. Pindi H. Chana ambaye alikuwa mgeni rasimi kwenye
mahafali yaliyofanyika Chuoni hapo (OUT) tarehe 20 Agosti, 2015.
Mapema mwezi Januri, 2015 Chuo Kikuu Huria
kwa ushirikiano na asasi ya ‘Nafasi Opportunity Society (NOS)’ ya nchini Canada
walibaini wasichana 22 wanaoishi katika mazingira hatarishi kutoka mikoa
mbalimbali na kuwapa fursa ya kujiunga na mafunzo ya ujasiriamali, ususi na
ulembo kwa lengo la kuwawezesha kupata stadi na weledi ili kuboresha kazi
zao. Katika kufanikisha lengo hilo asasi ya NOS ilikubali kugharimia
mafunzo ya wasichana hao kuanzia Januri 2015 hadi Agosti, 2015 na wote kuweza
kuhitimu na kutunukiwa vyeti na Mhe. Pindi Chana. Mgeni Rasimi Mhe. Pindi
aliwapongeza waliohitimu maana mafunzo waliyopata yamewaongezea mbinu katika
ajira.
Pili, wameweza kupata maarifa na stadi za
ujasiriamali hivyo kuwawezesha kujiajiri na kuajiri wengine. Fursa ya mafunzo
waliyopata wasichana itaongeza thamani ya utumishi wao katika soko la ajira
maana wamepata mafunzo kutoka katika Chuo makini (OUT) na huduma ya wahitimu
hao itawawezesha kupata kazi zenye staha katika soko na watatangazia vizuri
nafasi ya Chuo Kikuu Huria Tanzania katika kumwendeleza mwanamke. Mhe. Pinda
alisisitiza kuwa elimu ya urembo ni fani ambayo inahitajika kwa wanaume na
wanawake wa vijijini na mijini. Kama fani hii ya urembo itaendelezwa itaongeza
nafasi za ajira kwa wasichana na wavulana kwa kiasi kikubwa maana mahitaji yake
ni ya hakika katika soko.
Awali Kaimu Mkuu wa Chuo Huria cha Tanzania
Prof. matern Victor, alieleza kuwa mafunzo hayo maalum kwa wasichana wanaoishi
katika mazingira magumu yalilenga kujenga uwezo wa familia na jamii katika
mikoa na kwamba kama rasilimali fedha ikipatikana na jamii ikaendeleza juhudi
za kutoa haki sawa ya elimu kwa wote wasichana wengi wenaweza kufikiwa kupitia
Ofisi za mikoa.
Toa maoni yako hapa.
0 comments:
Post a Comment