Mhe. Shaban Ali Lila, Jaji Kiongozi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania (katikati) akitoa neno la utangulizi katika Semina ya
Mafunzo elekezi kwa Wahe. Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya Tanzania walioapishwa
hivi karibuni, aliyeketi kushoto ni Mhe. Anold Nsekela, Jaji Mstaafu wa
Mahakama ya Rufani (T) kulia ni Mhe. Salvatory Bongole, Kaimu Jaji Mfawidhi
wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
Mhe. Jaji Ferdinand Wambali
(aliyesimama), Mkuu wa Chuo cha Mahakama Lushoto (IJA),akitoa mada juu ya
utendaji kazi katika Mahakama katika mafunzo yaliyoanza kufanyika mapema leo
katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa (JNICC) jijini Dar es Salaam
Mhe. Shaban Ali Lila, Jaji Kiongozi- Mahakama
Kuu ya Tanzania (katikati) Mhe. Anold Nsekela, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani
(T), Mhe. Salvatory Bongole, Kaimu Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Majaji wapya wa Mahakama Kuu ya
Tanzania walioapishwa hivi karibuni, Majaji hao wapo katika mafunzo elekezi
yenye lengo la kuwawezesha sheria mbalimbali na taratibu za Kimahakama. Mafunzo
haya yataendelea kufanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA)
kuanzia tarehe 24.08.2015 ambapo mada mbalimbali zitatolewa ili kuwawezesha
Wahe. Majaji hao kuifahamu Mahakama, ikiwa ni pamoja na misingi na
taratibu za utoaji huduma ya haki nchini.
0 comments:
Post a Comment