Tuesday, 25 August 2015

#YALIYOJIRI>>>MTANGAZAJI WA BBC DIRA YA DUNIA SALIM KIKEKE ATEMBELEA OFISI ZA MICHUZI BLOG JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

 Mtangazaji nguli  wa kipindi cha BBC Idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke alipotembelea katika ofisi za MICHUZI MEDIA GROUP (MMG), leo jijini Dar es Salaam. Michuzi Blog ni blog pekee duniani ambayo BBC dira ya dunia imeichagua kushirikiana nayo katika kuendeleza libenke la habari ambapo kila siku kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kipindi maarufu cha habari cha Dira ya Dunia hurushwa na Globu ya Jamii. Pamoja na mambo mengi mengine Kikeke ameipongeza Michuzi Blog kwa kuendelea kuwa kinara wa habari za uhakika kwa Kiswahili zinazosomwa zaidi duniani, pia ameipongeza blog hiyo kwa kutimiza miaka 10 ya huduma za uhakika toka ilipoanza Septemba 8, 2005 jijini Helsinki Finland. Mahojiano na Salim Kikeke yatakujia karibuni ikiwa ni moja ya shamrashamra za kusherehekea miaka 10 ya Michuzi Blog. Stay tuned!
   Mtangazaji kinara wa kipindi cha BBC idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Michuzi Media Group jijini Dar es Salaam leo.
Mtangazaji nguli  wa kipindi cha BBC Idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke akifanya mahojiano na mwandishi wa  Michuzi tv online na  Michuzi Blog, Chalila Kibuda,   jijini Dar es Salaam leo.
 Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Michuzi Media Group, Muhidini Issa Michuzi,Mpiga picha za Video, Bakari Issa Majeshi,Mtangazaji nguli wa kipindi cha BBC idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke, Mwandishi wa habari, Chalila Kibuda, Mwandishi wa habari na Mpiga picha Avila Kakingo na Mdau Mpondela  wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanya mahojiano na Mtangazaji huyo wa BBC leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Michuzi Media Group, Muhidini Issa Michuzi, akiwa  na Mtangazaji kinara wa kipindi cha BBC  idhaa ya Kiswahili cha Dira ya Dunia, Salim Kikeke jijini Dar es Salaam leo.

0 comments:

Post a Comment