Na Yusuph Kileo Zikiwa zimebaki siku chache
kuanza kutumika kwa sheria mtandao Nchini Tanzania, Mengi yame endelea
kuzungumzwa ikiwa ni pamoja na kurudia mapungufu yaliyopatikana katika sheria
ya awali iliyo wasilishwa bungeni na kusambazwa kwa maneno kua sharia hii mtandao
ipo kuziba watanzania midomo huku wengine wakizungumzia itakiuka faragha za
watanzania. Sheria hii inakuja kusaidia mambo mengi na ni wazi mengi hayo
yamekua hayazungumzwi kabisa. Hivi karibuni kupitia mkutano mkuu wa mwaka wa
maswala ya usalama mitandao ambapo moja ya mijadala iliangazia sharia hii na
kutolea ufafanuzi yale yaliyokua hayajaeleweka vizuri. Binafsi Nilikua mmoja wa
washiriki ambapo kwa ujumla wetu tulianisha mambo kadhaa na kuzidi kutoa hofu
kwa yale ambay yameendelea kupotoshwa kuelekea matumizi ya sharia hii mtandao.
Makala hii itajikita kwenye hayo yasiyo zungumzwa kwa wingi hivi sasa. Upotevu
wa fedha, hivi karibuni akizungumza na Jeshi la polisi waziri wa
Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa alitahadharisha kua shilingi
trilioni 54.4 zitakuwepo kwenye hatari ya kuingia katika mikono ya wahalifu wa
mitandao, endapo Sheria za Mitandao na Miamala ya fedha haitatumika. Alianisha
kua fedha hizo ni sawa na trioni 4.4 kila mwezi. Profesa Mbarawa amesema fedha
hizo lazima zilindwe kwa kuwekewa sheria zenye kuzuia na kutoa adhabu kwa
watu watakaoingilia mihamala ya fedha. Kuzilinda fedha hizo Sheria mtandao
haina budi kuwepo ili kuwapa uwezo wahusika kufanya kazi yao ipasavyo.
Chanzo
Michuzi
0 comments:
Post a Comment