*Januzaj ajiunga na Borussia Dortmund
*Javier Hernendez aenda Bayer Leverkusen
*De Gea atua Real Madrid
*Man U wamnasa Martial kutoka Monaco
* Borini njiapanda, Jelavic ni West Ham
Hatimaye
Manchester City wamekamilisha usajili wa kiungo waliyekuwa wakimsaka
kwa udi na uvumba, Kevin De Bruyne kutoka Wolfsburg, kwa ada ya uhamisho
ya pauni milioni 55.
De Bruyne, 24, amesaini mkataba wa
miaka sita Etihad na anakuwa mchezaji wa nne mkubwa kusajiliwa kiangazi
hiki, baada ya Raheem Sterling kutoka Liverpoo na Timu ya Taifa ya
England, Fabian Delph wa Aston Villa na mchezaji wa kimataifa wa
Argentina, Nicolas Otamendi aliyekuwa Valencia.
De Bruyne
ni mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji, ambaye anakuwa wa pili aghali
katika usajili kwa klabu za England, nyuma ya Angel Di Maria
aliyesajiliwa kiangazi kilichopita na Manchester United kwa pauni
milioni 59.7 kutoka Real Madrid, akashindwa kung’ara na sasa ameuzwa
Paris Saint-Germain (PSG).
Kocha wa Manchester City,
Manuel Pellegrini alionesha furaha yake kumpata mchezaji huyo, na
alikuwa na haya ya kusema kumhusu: “Inabidi uwe na mchezaji wa kipekee
ili kuboresha kikosi. Sisi hupenda mchezo wa kushambulia sana na
unaovutia, kwa hiyo kusajili mchezaji kama huyu utakuwa msaada mkubwa
sana kwetu. Ana kila tunachohitaji – utimamu wa mwili, akili, ufundi na
mbinu zinazotakiwa uwanjani.”
De Bruyne aliyekuwa Chelsea
kabla ya kutupwa kwa madai hana kiwango, amesema anataka kufika katika
kilele cha mafanikio kwa maana ya kiwango cha juu cha uchezaji soka huku
akiwapatia klabu yake mataji. Amepewa jezi
Picha zaidi hizi hapa.
0 comments:
Post a Comment