Kikosi cha Azam FC chini ya
Stewart John Hall kimerejea jana toka visiwani Zanzibar kilikoweka kambi ya
wiki moja kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Jumamosi
tarehe 22/08/2015
Azam FC ambao ni mabingwa wa
CECAFA Kagame Cup, wamepania kuhakikisha wanatwaa Ngao hiyo ambayo mara tatu
wameipoteza dhidi ya Simba na Yanga.
Kikosi cha Azam FC kimeimarika
sana baada ya kurejea Stewart Hall ambaye amejenga ngome imara ya ulinzi huku
akibadilisha mfumo wa uchezaji toka 4-3-3 uliozoeleka na sasa Azam FC inacheza
mfumo wa 3-5-2
Azam FC ambayo kwenye mashindano
ya CECAFA ya Kagame Cup iliwakosa nyota wake kadhaa kama Allan Wanga na
Ramadhan Singano Messi, imejipanga kuhakikisha inashinda kila kikombe kilicho
mbele yake.
Chanzo
Azam Fc
0 comments:
Post a Comment