Monday, 24 August 2015

#YALIYOJIRI>>>Rais wa Zanzibar Dr Shein amekanusha kuwepo makubaliano na upande wa upinzani kuvunja tume ya uchaguzi Zanzibar.



Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein amekanusha kuwepo kwa makubaliano na upande wa upinzani wa kuivunja tume ya uchaguzi ya Zanzibar.
Dr Shein ametoa msimamo huo hapa Zanzibar wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania urais wa Zanzibar kupitia CCM ambapo zoezi hilo la uchuakuji fomu lilifanyika kwa kishindo cha wanaccm ambao waliambatana na Dr Shein kukabidhiwa fomu hiyo na mwenyekiti wa tume ambapo Dr Shein alisema hakuna upungufu wowote aliouna ndani ya tume hiyo na yeye kama rais hana malaka ya kuingilia utendaji wa tume hiyo.

Akizungumzia uchaguzi mkuu unaokuja Dr Shein amewalaumu wale ambao wanadai CCM ushindi wao unatokana na kuiba kura amesema hilo ni kosa kubwa na yeye kama kiongozi wa chama halikubali na halitokubaliwa  kwa vile CCM inashinda kihalali.

Baadaye Dr Shein alianza msfara wa kuelekea ofisi kuu ya CCM akiwa katika gari la wazi na kusababisha shughuli za kiuchumi na biashara kusimama darajani wakati msafara huo ukipita Dr Shein anakuwa mgombea wa 11 kuchuka fomu ya urais wa Zanzibar na siku ya mwisho ni tarehe 6 Septemba.
Chanzo
                                                   BBC SWAHILI.
                             

0 comments:

Post a Comment