Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro sasa itaondoka nchini siku ya jumapili
usiku kuelekea Istambul nchini Uturuki kwa kambi ya siku nane kujiandaa na
mchezo dhidi ya Nigeria Septemba 05, 2015.
Awali
Taifa Stars ilikua ipitie Muscat nchini Oman kucheza mchezo wa kirafiki na timu
ya taifa ya nchi hiyo, lakini kutokana na shirkikisho la Soka la Oman kushindwa
kukidhi mahitaji ya Kanuni za FIFA za uuandaaji wa mechi ya kimataifa ya
kirafiki sasa mchezo huo hautakuwepo tena.
Stars inatarajiwa kuondoka jumapili usiku na
shirika la ndege la Uturuki (Turkish Airlines) na kuwasili Istambul (Ataturk
Airport) siku ya jumatatu majira ya saa 5 kamili asubuhi, kisha kuelekea Kocael
katika hoteli ya Green Park Kartepe ambapo ndio itakua kambi yake ya wiki moja.
UCHAGUZI WA TEFA WAAHIRISHWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF)
kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Aloyce Komba imeitisha majalada ya
kamati ya uchaguzi ya TEFA na kamati ya uchaguzi ya DRFA baada ya kupokea
malalamiko na rufaa kutoka kwa wagombea.
Kamati ya Uchaguz ya TFF imeyaomba majalada
hayo ili ijiridhishe na kuona haki inatendeka kwa wagombea wote na baadae
tarehe mpya ya uchaguzi itatolewa.
SAANYA KUCHEZESHA AZAM NA YANGA
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF)
limemteua mwamuzi wa kati Martin Saanya kuchezesha mchezo wa Ngao ya Jamii
jumamosi, badala ya mwamuzi Israle Nkongo aliyekua amepangwa awali.
Mwamuzi Israel Nkongo anasumbuliwa na
matatizo ya misuli ya paja, ambayo itampelekea kukaa nje ya uwanja kwa
takribani siku kumi, hali iliyopeleka TFF kumbadilisha mwamuzi huyo kuelekea
kwenye mchezo huo wa jumamosi.
0 comments:
Post a Comment