Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepokea boti mbili za kisasa za kuhudumia meli kutoka China zitakazotumika katika Bandari za Dar es Salaam na Tanga.
Meneja Mawasiliano wa TPA, Janeth
Ruzangi alisema ujio wa boti hizo zilizopolewa jana utasaidia kuongeza
kasi ya utendaji kazi na ufanisi katika bandari hizo.
Alisema ujio wa
boti hizo ni sehemu ya mkakati wa TPA kuongeza vitendea kazi kwa upande
wa majini na nchi kavu ili kuongeza kasi ya upakuaji na upakiaji wa
mizigo kwa kiwango cha kimataifa na hivyo kuvutia wateja wengi.
Nahodha
Mkuu wa TPA, Kapteni Abdullah Mwingamno alisema boti ya tani 70
iliyopewa jina la Valeria Rugaihuruza itabaki Dar es Salaam kwa ajili ya
kuhudumia meli zinazoshusha mafuta katika Boya la SPM lililopo Mji
Mwema, wakati nyingine inayoitwa Mwambani itapelekwa Bandari ya Tanga
kwa ajili ya kuhudumia matishari.
Boti ya MV Valeria Rugaihuruza
imeundwa na ‘crane’ yake pamoja na boti nyingine ndogo mbili ndani yake
kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi kwenye boya la mafuta. Boti ya MV
Mwambani ina uwezo wa kuvuta tishari lenye uwezo wa kubeba tani 3,500 za
mizigo.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment