Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, jana amesaini sheria ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ya Zanzibar.
Mbali ya kusaini sheria hiyo, amewapiga kijembe wanaoikosoa sheria hiyo kuwa ni wachoyo na wasioitakia mema Zanzibar.
Dk.
Shein aliwaambia viongozi na waandishi wa habari kuwa sheria hiyo namba
6 ya mwaka 2016, inaipa Zanzibar mamlaka ya kisheria ya kuendeleza
rasilimali ya mafuta na gesi asilia.
Alisema kitendo cha kutia saini sheria hiyo, hakijavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano kama baadhi ya watu wanavyodai.
“Hakuna
aliyevunja sheria, anayevunja sheria wala atakayevunja sheria. Lakini
kama wao wanadai kutia saini sheria hii ni kuvunja sheria, basi watafute
suluhisho la kisheria,” alisema.
Aliwashauri
wenye mawazo hayo wakasome vizuri Sheria ya Mafuta Namba 21 ya 2015
iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo
imeweka msingi imara wa kisheria wa kutambua rasilimali ya mafuta na
gesi asilia ni miongoni mwa mambo yaliyoorodheshwa kwenye Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yanahitaji usimamizi bora na
imara wa kisheria.
Alisema
sheria hiyo imeainisha mambo makuu matatu ambayo kwanza ni kuwa
shughuli zote za mafuta na gesi asilia kwa upande wa Tanzania Bara
zitasimamiwa na taasisi zilizoanzishwa ndani ya sheria namba 21 ya 2015.
Sheria
hiyo inatamka pia kuwa shughuli zote za mafuta na gesi asilia kwa
upande wa Tanzania Zanzibar zitafanywa na taasisi zitakazoanzishwa kwa
mujibu wa sheria za Tanzania Zanzibar.
Kuhusu
mapato yatokanayo na shughuli hizo, Dk. Shein alisema sheria inatamka
upande wa Tanzania Bara mapato yatatumiwa na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa faida ya Tanzania Bara wakati kwa upande wa
Tanzania Zanzibar yatatumiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
faida ya Zanzibar.
“Kila
upande ulishiriki kikamilifu katika mchakato huu. Tulishauriana kwa
kina viongozi na tukapata ushauri wa kutosha kutoka kwa wanasheria wetu
wakuu hadi kufika bungeni,” alisema Dk. Shein.
Alisema
anatambua sheria hiyo ni mpya na anaelewa changamoto ambazo zinaweza
kutokea, lakini akatoa wito kwa wananchi kuiunga mkono na kushirikiana
na Serikali.
“Mafuta ni jambo kubwa katika maendeleo, pia yasipotumika vyema yanaweza kuitikisa nchi,” alisema Dk. Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha hati muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,baada ya kusaini hati hiyo katika hafla iliyofanyika jana ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya Siasa walihudhuria hafkla hiyo,[Picha na Ikulu.] Viongozi Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja. Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi na Viongozi mbali mbali wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja jana. Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid (kulia) na Waziri wa Nishati na Madini Mhe,Profesa Sospiter Muhongo,wakiwa katika hafla ya Utiaji wa saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja jana.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment