Katikati Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akishiriki katika kuteketeza tanuru la mkaaa katikati ya hifadhi ya m situ ya Mkwemu Wilayani Kahama.
Na Evelyn Mkokoi
Hifadhi
ya Taifa ya Msitu wa Ukwemi uliyopo katika wilaya ya Kahama upo
hatarini kutoweka kutokana na shughili za kibinadamu zinazofanywa ndani
ya hifadhi hiyo zinazochangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.
Hayo
yameelezwa na Meneja kutoka wakala wa Taifa wa Misitu Bw. Mohamed Dosa
wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. Luhaga Mpina alipotembelea HIfadhi hiyo iliyopo ndani ya
Halmashauri ya Kahama inayopakana na Halmashauri ya Mbongwe Mmkoani
geita.
Katika
Ziara yake ya Ukaguzi wa Mazingira katika Hifadhi ya Msitu Huo, Naibu
Waziri Mpina alielezwa kuwa shughuli kubwa zinazotegemewa na wakazi wa
vijiji vya jirani na msitu huo ni, ukataji miti kwa uchomaji wa mikaa na
ukataji wa magogo kwa shunghuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na shughuli
na ujenzi na utengenezaji wa samani za majumbani.
Meneja
Dosa Amemuelezea Naiubu Waziri Mpina kuwa (generation) kizazi cha
kwanza cha aina na miti ndani ya hifadhi hiyo kilishakwisha na miti
inayoota na kuonekana sasa ni ya kizazi cha pili.
“changamoto
kubwa tunayokumbana nayo katika kulinda hifadhi hii ni magari ya doria
kuzunguka ndani ya msitu kwani ni mkubwa sana na hakuna skari wa kutosha
kufanya doria. “ Alisisitiza Bw. Dosa.
Akiwa
katikati ya Msitu huo Naibu Waziri Mpina alijionea Uharibifu mkubwa wa
uchomaji mkaa na kushuhudia mhalifu Bw John Abdalah Sanga makazi wa
kijiji cha jirani cha mwendakulima aliyekuwa akimaliza kuchoma mkaa
katikati ya msitu huo na kueleza kuwa amekuwa akifanya kazi hiyo kwa
takribani miaka mitatu sasa hali iliyompelekea Naibu Waziri Mpina na
timu yake kutekekeza baadhi ya matanuru ya mkaa ndani yam situ huo.
Kwa
upande wake Mratibu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa
Mazingira NEMC kanda ya ziwa Bw. Jamal Baruti alieleza kuwa hali ya
uharibifu wa misitu nchini bado ni kubwa na suala la mkaa bado ni
changamoto, hivyo wanaanchi washiriki katika kuhifadhi misitu na
kutafuta mbadala wa mkaa na misitu ni muhimu kwa kutunza baiyonuwai.,
wakati katibu tawala wa wilaya ya kahama Bw. Thomas Nganya akitoa Rai
kwa wananchi waone kuwa suala la utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila
mmoja na siyo kuiachia seriali peke yake.
Aliyeshika
kiuno, Naibu Waziri Ofisi Ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina akiangalia Tanuru la Mkaa likitekea baada ya kushiriki
kuteketeza ndani ya Msitu wa Mkwemu wilayani Kahama.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment