Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haitawavumilia waajiri ambao
hawatoi mikataba ya ajira kwa wafanyakazi wao na amewaonya waache tabia
hiyo mara moja.
Ametoa
agizo hilo jana (Jumatano, Novemba 23, 2016) wakati akifungua Mkutano
Mkuu wa Sita wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA)
katika ukumbi wa Mwalimu Julius K. Nyerere ulioko Chuo cha Mipango, nje
kidogo ya mji wa Dodoma.
Akijibu
hoja ya waajiri kutokutoa mikataba ya ajira kwa wafanyakazi ambayo
iliibuliwa kwenye risala yao, Waziri Mkuu alisema kifungu cha 14 cha
Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya mwaka 2004 kinaelekeza
aina mbalimbali za mikataba inayotakiwa kutumika kuajiri wafanyakazi.
“Kisheria mwajiri anao wajibu wa kuhakikisha kila mtumishi wake ana mkataba wa kazi kwa maandishi,” alisisitiza.
Akijibu
hoja kuhusu wafanyakazi kuwekwa ndani kiholela, kunyanyaswa, kushushwa
vyeo na kusimamishwa kazi na wanasiasa, Waziri Mkuu alisema Serikali
chini ya uongozi wa Dkt. John Pombe Magufuli itaendelea kuzingatia
utawala wa sheria na kanuni za utawala bora ili kuhakikisha kuwa haki za
wafanyakazi zinalindwa ipasavyo.
”Kimsingi
watumishi wanasimamiwa na mamlaka za kinidhamu na sheria mbalimbali
ambazo hazina budi kuangaliwa kwa pamoja kabla ya kuchukua hatua.
Ninawaagiza viongozi wenzagu wa kisiasa na walioko katika wizara na
taasisi zote za Serikali, mikoani, wilayani, kwenye idara za Serikali na
Halmashauri wazingatie utawala wa sheria wakati wa kushughulikia
masuala mbalimbali yanayohusu wajibu na haki za wafanyakazi,” alisema huku akishangiliwa.
Akijibu
hoja kuhusu suala la watumishi kutopandishwa vyeo, Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Bibi Angella Kairuki alisema kwa
kipindi cha miaka mitano jumla ya watumishi 343,689 walipandishwa vyeo
ikiwa ni kuanzia mwaka 2011 hadi 2016. Hata hivyo, alisema wanakabiliwa
na changamoto ya watumishi wengine kutokidhi vigezo.
“Kuna
baadhi ya watumishi hawakidhi vigezo vya maendeleo na masharti vya
muundo wa masharti ya utumishi wa umma. Tumetoa maelekezo kuwa wale
waliokosa vigezo na wamekaa muda mrefu bila kupandishwa vyeo, wapewe
mafunzo na bajeti zitengwe ili waweze kutimiza vigezo vya muundo wa
utumishi wa umma,” alisema.
Sauti ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment