Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema Uwanja wa
Nyamagana ambao umewekewa nyasi bandia ni juhudi za watu kadhaa, lakini
kodi ya wananchi wa mkoa wa Mwanza ndiyo iliyotoa mchango mkubwa kufikia
ulipo sasa.
Nape
ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kuutembelea uwanja huo
iliyofanyika leo jijini hapa baada ya serikali ya awamu ya tano
kuonyesha juhudi za makusudi kuhakikisha suala la upatikanaji wa nyasi
bandia, zinatolewa bandarini na kuwekwa kwenye uwanja huo linafanikiwa
kwa wakati mwafaka ili Mwanza na mikoa ya jirani ijiendeleze kimichezo
na hasa soka.
Akizungumza
na HEBRON MALELE wakati wa mkutano huo wa waandishi wa habari, Nape ambaye
ameonyesha kufuatilia mambo mengi ya michezo kwa ukaribu, amesema
wanaoutumia uwanja huo kama kampeni za kuwania uongozi hawako sawa kwa
kuwa si uwanja wa mtu, badala yake ni uwanja wa Wanamwanza.
“Huu
ni uwanja wa Wanamwanza wote, mama mtilie, wachuuzaji wa vitu
barabarani na wengine wamelipa kodi yao na serikali imeitumia katika
ununuzi wa nyasi bandia.
“Nyasi
hizo zilikwamba bandarini kutokana na suala la kodi. Lakini mwisho,
serikali ikashirikiana na TFF na kuzitoa na kazi ya uwekaji nyasi hizo
hii inakwenda ukingoni,” alismea.
Hivi
karibuni, kumekuwa na baadhi ya viongozi wa TFF na wale wa vyama vya
soka katika mikoa, wakiutumia kama sehemu ya kampeni zao za kuwania
kupata uongozi.
Pamoja na kutembelea uwanja huo, Nape aliwataka Wanamwanza kuutunza na kuudhamini kama sehemu ya moja ya maendeleo.
Aidha,
alisisitiza Serikali itaendelea kuwekeza kwa kufanya ukarabati kwenye
viwanja mbalimbali nchini ili kuviboresha na kusaidia kusukuma maendeleo
ya michezo kwa haraka zaidi.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment