Mahakama nchini Misri imebatilisha hukumu ya kifo aliyopewa rais aliyepinduliwa Mohammed Morsi.
Morsi alikumiwa kifo baada ya kulaumiwa kuhusika na kutoroka kwa wafungwa wengi wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011.
Alichaguliwa kuwa rais mwaka 2012 lakini akaondolewa na jeshi mwaka mmoja baadaye, kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake.
Morsi amewahi hukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mashtaka yanayohusu ugaidi na bado anakabiliwa na mashtaka kwa makosa mengine.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment