UONGOZI
wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, unayofuraha
kuwaataarifu wapenzi wa soka kuwa jioni ya leo umefanikiwa kuingia
mkataba wa miaka mitatu na kiungo mshambuliaji kutoka Ghana, Enock Atta
Agyei.
Agosti
mwaka huu, Azam FC tuliingia makubaliano maalumu na Medeama ya Ghana juu
ya kumsajili kinda huyo anayetimiza umri wa miaka 18 mwakani baada ya
benchi la ufundi kuridhishwa na uwezo wake na sasa amejiunga rasmi
kwenye viunga vya Azam Complex.
Agyei
anasaini mkataba tayari kabisa kuanza kuitumikia Azam FC katika mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) mwakani pamoja na
michuano mingine ikiwemo Kombe la Shirikisho Afrika.
Tunaamini
ya kuwa ujio wa nyota huyo wa timu ya Taifa ya Vijana ya Ghana chini ya
miaka 17, utazidi kuipa nguvu timu yetu kuelekea kwenye michuano
inayotukabili mbeleni, hivyo tunapenda kumtakia mafanikio mema kwa
kipindi chote atakachokuwa akiipigania jezi ya Azam FC.
Azam FC
tunapenda kuwafahamisha mashabiki wetu kuwa tutaendelea kukifanyia
marekebisho kikosi chetu kuelekea usajili wa dirisha dogo, lengo ni
kukipa nguvu kikosi hicho ili kifanye vizuri zaidi katika michuano ya
hapa nchini pamoja na ile ya Kimataifa.
Lengo
kubwa la Azam FC ni kuendelea kuwafurahisha mashabiki wetu kwa kupata
matokeo bora uwanjani, na tunaamini ya kuwa, benchi zuri la ufundi
tulilokuwa nalo, wachezaji wazuri walioko kikosini na wengine
watakaokuja kuongeza nguvu, wote kwa pamoja wataweza kutuvusha kuelekea
safari ya mafanikio msimu huu.
Hivyo,
tunawaomba mashabiki wetu kuvuta subira na kuendelea kuisapoti timu
kwani tunaamini ya kuwa nyie ndio nguzo muhimu ya 12 uwanjani katika
kuwapa hamasa wachezaji ya kupata matokeo bora pamoja na kuijenga timu
kiujumla.
Wakati
huo huo, leo tumewapokea wachezaji saba waliokuja kwenye majaribio ya
kujiunga na Azam FC, ambao ni mabeki wa kati Mbimbe Aaron Nkot
(Cameroon), Kone Nabil Ibrahim (Ivory Coast), kiungo mkabaji Kingue
Mpondo Stephane (Cameroon),
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment