Mikoa ya Tabora, Katavi na Rukwa imetajwa kuwa ni miongoni mwa mikoa 10 inayoongoza kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011/2012 za Taasisi ya Mkapa.
Taarifa
hiyo ilitolewa na Meneja Mradi wa TB na Ukimwi kutoka Taasisi ya
Mkapa, Dkt. Happenes Wilbroad katika mafunzo ya siku moja ya
viongozi wa dini yaliyofanyika Nzega.
Alisema
mkoa unaoongoza kwa maambukizi ya VVU kati ya mikoa hiyo mitatu ni
Rukwa wenyeasilimia 6.2 ukifuatiwa na Katavi asilimia 5.2 na Tabora
asilimia 5.1.
Dk.
Wilbroad alisema Taasisi ya Mkapa imeanza kuendesha mafunzo ya
kuhakikisha wananchi wanatambua na kuepuka maambukizi mapya.
Alisema jitiahada mbalimbali za kudhibiti maambukizi hayo zinapaswa kufanyika kunusuru maisha ya wakazi wa maeneo hayo.
Alitaja
sababu zinazochangia maambukizi kuwa ni pamoja na ndoa za utotoni,
tohara za jadi na baadhi ya wananchi kutozingatia elimu ya Ukimwi na
kukithiri imani potofu za ushirikina.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment