Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa viwango vya ubora wa vilabu barani Africa ambapo timu za Tanzania zimeendelea kutokuwa kwenye namba nzuri zaidi ambapo Yanga inayoongoza kwa timu za Tanzania imeshika nafasi ya 331.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania Yanga SC imeshika nafasi ya 331 huku Azam FC ikishika nafasi ya 351na Simba ikiwa nafasi ya 356.
Yanga wamepata pointi nyingi kutokana na ushiriki wao katika michuano ya CAF wakivuka raundi ya pili klabu bingwa Afrika msimu wa 2015-16 na kufika hatua ya nane bora kombe la Shirikisho.
Etoile du Sahel ya Tunisia ndio inaongoza ikifuatiwa na TP Mazembe ya DR Congo huku Esperance de Tunis ikishika nafasi ya nne mbele ya Vita Club ya DR Congo na Al-Merreikh ya Sudan ikifunga tano bora.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment