WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Jiji la Dar es Salaam watumie fursa ya uwepo wa umeme wa uhakika kwa kuanzisha viwanda vidogo na vikubwa ili waweze kujiongzea kipato.
Ametoa wito huo jana (Jumatano, Novemba 16, 2016) wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa mradi wa uboreshaji miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam uliofanyika kwenye Ofisi za TANESCO zilizoko Mikocheni jijini humo.
Akizungumza kabla ya kubonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi huo, Waziri Mkuu alisema:
“Umeme ni mhimili mkubwa sana kwa maendeleo ya nchi yoyote ile.
Tumepata umeme wa uhakika, tumieni fursa hii ya uwepo wa umeme wa
uhakika kujiongezea kipato.”
“Hivi
sasa tumepata umeme wa uhakika, fanyeni kazi kwa bidii ili mfaidi
matunda ya kuwepo kwa umeme huo. Serikali inategemea kwamba sasa
wananchi mtaanzisha na kukuza viwanda vidogo vidogo na vikubwa, biashara
zitapanuka na kilimo bora huko vijijini kitaongezeka,” alisema.
Alisema
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda na moja
ya nyenzo kuu ya kuendesha uchumi wa viwanda kwa tija na ufanisi ni
upatikanaji wa nishati ya umeme ya uhakika, na ndiyo maana kwa
kushirikiana na wadau wa maendeleo Serikali imefanya jitihada kubwa
kuhakikisha miundombinu ya umeme inaboreshwa ili kuondoa tatizo la
kukatika kwa umeme.
“Wataalam
wamenieleza kuwa mradi huu ulihusisha ujenzi wa kituo kikubwa cha
kupozea umeme cha MVA 100, ujenzi wa njia za usafirishaji umeme wa
msongo wa kilovoti 132 katika maeneo mbalimbali ya Jiji kupitia chini ya
ardhi, ujenzi wa njia za usambazaji umeme wa msongo wa kilovoti 33,
pamoja na ujenzi wa ujenzi kituo cha udhibiti mifumo ya usambazaji umeme
(Distribution SCADA System) katika msongo wa kilovoti 33 na 11.”
“Kukamilika
kwa mradi huu kunaondoa adha zilizokuwepo awali kutokana na kukatika
umeme mara kwa mara. Jiji la Dar es Salaam ni kitovu cha shughuli za
biashara katika kuleta maendeleo ya Taifa ambapo upatikanaji wa umeme wa
uhakika ni wa lazima,” aliongeza.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na hadhira iliyokuwepo, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alisema
Wakala wa Jiolojia Tanzania kwa kushirikiana na Wakala wa Jiolojia wa
Finland wanaunda mpango wa pamoja wa kuibua madini ya kisasa ambayo
yanatafutwa zaidi duniani kukidhi mahitaji ya kiteknolojia.
“Hivi
sasa madini kama graphite na lithium yanahitajika zaidi kwenye
teknolojia za kisasa kama za utengenezaji wa simu, tuachane na madini
yaliyozoeleka kama vile dhahabu na Tanzanite,” alisisitiza.
Alitumia
fursa kuuagiza uongozi wa TANESCO uhakikishe kuwa hakuna mgao wa umeme
nchi nzima kwani Watanzania wamechoshwa na tabia ya kukatiwa umeme mara
kwa mara.
“Ili tujenge nchi ya viwanda, tunahitaji umeme wa uhakika, umeme unaotabirika na zaidi ya yote umeme wa bei nafuu,” alisema huku akishangiliwa.
“Ili tujenge nchi ya viwanda, tunahitaji umeme wa uhakika, umeme unaotabirika na zaidi ya yote umeme wa bei nafuu,” alisema huku akishangiliwa.
Naye
Waziri wa Biashara za Nje na Maendeleo wa Finland, Bw. Kai Mykkanen
alisema Serikali yake imedhamini ujenzi wa mradi huo kwa vile inaamini
kuwa umeme wa uhakika ni suluhisho la kuondoa umaskini kwa hiyo
kukamilika kwa mradi huo kutaondoa adha ya kukatika umeme kila mara.
Aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika eneo la nishati ya umeme na nishati mbadala.
Katika
hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Eng. Felchesmi Mramba
alisema ujenzi wa mradi huo umegahirimu sh. bilioni 74.6 ambapo kati ya
hizo, sh. bilioni 63.56 zimetolewa na Serikali ya Finland na sh. bilioni
11.03 zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
Alisema
kukamilika kwa mradi huo kumewezesha sehemu kubwa ya Jiji la Dar es
Salaam kuwa na njia za mzunguko (ring circuit) zinaoingizaa umeme.
“Teknolojia hii iliyotumika itawezesha vituo vya kupozea umeme kuwa na njia mbadala ya kupata umeme endapo njia mojawapo inayopeleka umeme itapata hitilafu,” alisema.
“Teknolojia hii iliyotumika itawezesha vituo vya kupozea umeme kuwa na njia mbadala ya kupata umeme endapo njia mojawapo inayopeleka umeme itapata hitilafu,” alisema.
Naye
Meneja wa Kituo cha Kudhibiti Mifumo ya Usambazaji, Eng. Alex Kalanje
alimweleza Waziri Mkuu kwamba kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kompyta,
(distribution SCADA SYSTEM) kituo hicho cha udhibiti wa mifumo ya
usambazaji umeme katika jiji la Dar es Salaam kitawasaidia watoa huduma
wao waweze kufuatilia kwa haraka zaidi pale matatizo yanapotokea.
“Baada ya kukamilika kwa kituo hiki, lengo letu ni kujenga kituo kama hiki kwenye mjai ya Arusha, Mbeya, Dodoma na Mwanza,” alisema.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Biashara na maendeleo wa Finland,
Kai Mykkanen wakatizama moja ya mitambo ya umeme katika Kituo cha
TANESCO cha Mikocheni kabla ya kuzindua Mradi wa Uboreshaji Miundombinu
ya Umeme jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) wakitazama mfumo wa usambazaji umeme kabla ya Waziri Mkuu kuzindua Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini Dar es salaam kwenye Kituo cha TANESCO cha Mikocheni jijini Dar es salaam Novemba 16, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen akizungumza katika Uzindunduzi wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya umeme katika jiji la Dar es salaam uliofanywa na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kwenye Kituo cha TANESCO cha Mikocheni jijini Dar es salaam Novemba 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza katika Uzindunduzi wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya umeme katika jiji la Dar es salaam uliofanywa na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kwenye Kituo cha TANESCO cha Mikocheni jijini Dar es salaam Novemba 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini Dar es salaam kwenye Kituo cha TANESCO cha Mikocheni Novemba 16, 2016. Kushoto kwake ni Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen na kulia kwake ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini Dar es salaam kwenye Kituo cha TANESCO cha Mikocheni Novemba 16, 2016. Kushoto kwake ni Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen na kulia kwake ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watalaam kutoka Finland baada ya kuzindua Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini Dar es salaam kwenye Kituo cha TANESCO cha Mikocheni Novemba 16, 2016. Kushoto kwake ni Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen na kulia kwake ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri wa Biashara na Maendeleo wa
Finland, Kai Mykkanen baada ya kuzindua Mradi wa Uboreshaji Miundombinu
ya Umeme katika jiji la Dar es salaam kwenye Kituo cha TANESCO cha
Mikocheni Novemba 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
OFISI YA WAZIRI MKUU,
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment