Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa ufafanuzi kuhusu
kutoonekana kwake kwenye misiba ya viongozi wawili wa zamani serikalini,
Samuel Sitta na Joseph Mungai.
Sitta, aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa,
alifariki dunia Novemba 7, akiwa Ujerumani alikokwenda kutibiwa tezi
dume na siku iliyofuata alifariki Mungai, aliyekuwa Waziri wa Elimu wa
Serikali ya Awamu ya Tatu.
Gumzo kwenye mitandao ya kijamii lilikuwa ni kutoonekana kwa Lowassa, ambaye hivi sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.
Lowassa alisema kuwa, kilichomkwamisha kufika
kwenye misiba hiyo ni kuwa safarini Afrika Kusini alikokwenda
kumuangalia mdogo wake, Bahati Lowassa aliyekuwa mgonjwa.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment