Kiungo
kinda wa Simba, Said Ndemla, wakati wowote kuanzia sasa anaweza
kuachana na timu hiyo na kwenda Ulaya kutafuta nafasi ya kucheza soka la
kulipwa.
Meneja
wa kiungo hiyo, Jamal Kisongo, amesema hivi sasa yupo katika harakati
za mazungumzo na baadhi ya timu kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya
ambayo yameonyesha nia ya kutaka kumchukua mchezaji huo.
Alisema
endapo mipango hiyo itakaa sawa, muda wowote ataondoka nchini na kwenda
huko kujaribu bahati yake ya kucheza soka la kulipwa kama ilivyo kwa
mshambuliaji Mbwana Samatta anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya
Ubelgiji.
“Said
Ndemla muda wowote kuanzia sasa anaweza kuondoka zake nchini na kwenda
Ulaya kwa ajili ya kujaribu bahati yake ya kucheza soka la kulipwa kama
alivyo Samatta.
“Hivi
sasa nipo katika mazungumzo na baadhi ya timu ambazo zimeonyesha nia ya
kumtaka na endapo mambo yatakaa sawa basi ataondoka nchini kwa sababu
tayari ameshakomaa kiakili na kifikra, hivyo anaweza kupambana,” alisema
Kisongo.
Alipoulizwa
kama uongozi wa Simba unaujua mpango huo, alisema: “Simba wanaujua,
hivyo mambo yakikaa sawa ataondoka, wala hawana shida."
SOURCE: CHAMPIONI
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment