Siku
chache baada ya kuripotiwa taarifa za kukamatwa kwa mwanaume mmoja
kutoka Malawi ambaye inadaiwa alikuwa akiwanajisi watoto wadogo
wanaotajwa kufika 100 kwa maelezo kwamba anawasafisha na kufanya tambiko
la kimila, Hatimaye amehukumiwa kwenda jela miaka miwili.
Hukumu
hiyo imeonesha kutotenda haki kwa watoto hao kutokana na uchache wa
miaka aliyofungwa mwanaume huyo. Tayari mashirika ya kutetea haki za
binadamu na asasi za kupambana na maambukizi ya virusi vya HIV nchini
Malawi zimekosoa hukumu hiyo
Michael
Chipeta, wakili na mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini
humo amekosoa hukumu hiyo na kusema kuwa kulikuwa na mapungufu mengi
katika mchakato mzima wa kesi na hukumu dhidi ya mwathirika huyo wa
virusi vya HIV, anayejulikana kama Eric Aniva mwenye umri wa miaka 45.
Eric
Aniva alikiri kwamba amefanya ngono na wasichana wadogo kwa kulipwa
fedha ambazo ni dola nne mpaka saba za Marekani kwa kuondoa usichana wa
(kubikiri) kila mtoto mmoja, kwa imani kuwa ubikira ni mkosi na kwamba
kitendo hicho kinawasafisha watoto hao pamoja na jamii hiyo.
Malawi ni katika nchi zenye maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi duniani.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment