Wataalamu
mbalimbali wa sekta ya afya, sasa wataanza kusajiliwa na kupewa leseni
zitakazowatambulisha na zitakuwa na masharti maalumu.
Hayo
yamesema na Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Muhammad Kambi jana
Jumatano jijini Dar es salaam, wakati akifungua mkutano wa mwaka wa
Chama cha Wafiziotherapia (APTA).
Alisema
serikali imeanza mchakato wa kuipitia upya Sheria ya Madaktari wa
Tanganyika, ambayo itaongezwa sharti hilo pamoja na kuundwa kwa bodi
maalumu itakayosimamia maadili ya watumishi hao.
“Lakini
hivi sasa kuna taaluma nyingi ndani ya hii fani, kwa mfano ninyi
wataalamu wa fiziotherapia. Mpo lakini sheria haiwatambui, kwa maana
hiyo inakuwa vigumu hata kuwafuatilia. Ndiyo msingi wa kuipitia upya
sheria hii,” alisema.
“Katika
sheria mpya itakayoboreshwa, kila mtumishi atatakiwa kukata leseni.
Kila mtumishi atatakiwa kujiendeleza kielimu, kuongeza ujuzi ili aendane
na wakati uliopo kwa sababu mambo yanabadilika, kile ulichosoma jana
unahitaji kujifunza zaidi,” alisema.
Aidha
Kambi alisema tayari maboresho ya sheria hiyo yameshawasilishwa katika
Kamati ya Baraza la Mawaziri ya Katiba na Sheria na imeshapitiwa.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment