Monday, 5 December 2016

#YALIYOJIRI>>>>PICHA: Ajali ya Lori na Hiace Yaua Watu 9 na Kujeruhi 18.

Watu tisa wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Ifunda mkoani Iringa jana baada ya lori kugonga gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace. 

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema dereva wa lori hilo lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam, alishindwa kufunga breki na kuigonga Hiace hiyo iliyokuwa imeegeshwa pembeni ya barabara. 
“Lori limeharibika kabisa na Hiace pia imeharibika kabisa,” alisema Kamanda Masenza. 
“Lori hilo liliposhindwa kufunga breki liliigonga Hiace ambalo lilikuwa na abiria na kwenda mbele na kisha kugonga watembea kwa miguu,,” 
Masenza alisema katika ajali hiyo iliyotokea jana jioni, madereva wa magari hayo wote wamejeruhiwa na wamelazwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa pamoja na majeruhi wengine. 
“Dereva mmoja yupo chumba cha upasuaji kwa kuwa mguu wake umevunjika na mwingine yupo wodini,” alisema

Related Posts:

  • Kubenea Atoa Siku Mbili Serikali Kulifungulia Gazeti la Mwanahalisi. WAHARIRI wa Gazeti la MwanaHalisi linalomilikiwa na Mbunge, Saed Kubenea lililofungiwa na serikali wamekanusha taarifa ya serikali kuwa gazeti hilo linaandika habari za uongo, wamedai kuwa wao hawajawahi kuandika uongo n… Read More
  • Whatsapp Yafutwa China. Baada ya malalamiko ya muda mrefu ya serikali ya China juu ya mtandao wa ujumbe mfupi wenye kubeba mafaili ya Sauti, Picha na Video “WhatsApp” hatimaye imeuondoa rasmi nchini humo. Imeripotiwa kuwa mtandao wa WhatsA… Read More
  • Inasikitisha Binti wa Darasa la Tatu Apewa Mimba. Mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13 wa darasa la tatu katika shule ya msingi Makutano, kitongoji cha Igole kijiji cha Makutano wilayani Kilombero amelazimika kukatizwa masomo yake kwa kufukuzwa shule baada ya kupewa ujauz… Read More
  • Muziki wa Vigodoro Wapigwa Marufuku Tanga. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga R.P.C Benedict Michael Wakulyamba, amepiga marufuku Vigodoro ndani ya jiji hilo kutokana na vitendo hivyo kuhamasisha uhalifu. Akiongea ofisini kwake R.P.C Benedict amesema miongoni mwa vi… Read More
  • Uchaguzi wa Marudio CCM Hapatoshi Vurugu Zatanda. Vurugu zimeibuka katika uchaguzi wa marudio wa kumpata mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM (UVCCM) Wilaya ya Nyamgana baada ya wajumbe kutoka Kata ya Mahina kuzuiwa kuingia ukumbini kupiga kura wakid… Read More

0 comments:

Post a Comment