Meya
wa mji wa Clay nchini Marekani, Beverly Whaling amejiuzulu wadhifa huo
baada ya kuunga mkono maandishi yenye ubaguzi wa rangi kwenye facebook
dhidi ya mke wa Rais Barack Obama, Michelle Obama.
Meya
huyo aliingia matatani na kuamua kujiuzulu nafasi yake baada ya
kuonesha kufurahishwa na ‘post’ ya kibaguzi iliyoandikwa na Mkurugenzi
wa shirika moja la kutoa misaada, Pamela Taylor aliyelenga kubainisha
tofauti kati ya mke wa Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump, Melania na
mama Michelle Obama.
Taylor alimtusi Michelle akimfananisha na sokwe huku akimpamba Melania kuwa ni mrembo.
Meya huyo aliandika chini ya ujumbe huo wa kibaguzi, “Just made my day Pam.”
Zaidi
ya watu 200,000 wamejiandikisha mtandaoni ndani ya muda mfupi kupinga
ubaguzi huo na kuwataka Whaling na Taylor kujiwajibisha haraka.
Vitendo vya kibaguzi vimeripotiwa kuongezeka nchini humo tangu Trump alipotangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais.
Ingawa
kauli zake wakati wa kampeni zilikuwa na matamko tata, Trump amewataka
wafuasi wake kuacha mara moja vitendo vyovyote vya kibaguzi akisisitiza
kuwa yeye atakuwa rais wa Wamarekani wote.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment