Baada ya kuona rekodi mbalimbali zikitengenezwa hali halisi ya mchezo wa soka ni kuweka rekodi ambazo zitakuwa katika kumbukumbu mbalimbali, Ronaldo na Messi kila wanachofanya ni rekodi hata kama hajafunga muda mrefu watu huandika rekodi maana sio kawaida na akifunga kila siku rekodi maana anavunja rekodi za waliopita.
Tunakuletea timu 5 ambazo zimewafanyia kitu mbaya ama Lugha inayoeleweka ‘Humiliated’ timu nyingine katika michuano ya UEFA Champions League na unaweza ukashangaa maana kuna timu zimeshinda kwao ila zimefungwa goli nyingi katika mchezo uliofuata.
5.ARSENAL DHIDI YA INTER MILANI 2003
Mchezo huu wengi wapenzi na mashabiki wa Arsenal hawatousahau haswa baada ya timu hizi kukutana Novemba 2003 ambapo Inter Milan wameichakaza Arsenal mabao 3-0 London. Baada ya kurejea Sansiro Arsenal walibadilisha matokeo na kuwaumiza magoli 5-1 na kupita mchezo huo.
4.DEPORTIVO LA CORUNA DHIDI YA AC MILAN
Ilikuwa Robo fainali ambapo mchezo wa kwanza AC Milan imempasua La CORUNA mabao 4-1, mchezo wa pili ambao ulifanyika pale Municipal de Riazor Milani amekufa mabao 4-0 na ikawa kama maajabu vile, na huu ndio mchezo wa soka ulivyo.
3.AC MILANI DHIDI YA REAL MADRID 1988
Mchezo huu ulikuwa nusu fainli ya michuano hii Milan imefanya maajabu baada ya sare ya 1-1 pale Santiago Bernabeu lakini mchezo wa pili AC Milan amempasua Madrid mabao 5-0 hivyo kuifanya AC Milan kupita na kuingia fainali ya michuano hiyo.
2.BARCELONA DHIDI YA BAYERN MUNICH
Mchezo huu wengi vijana wa sasa naamini wameutazama na Bayern ikiikausha Barcelona, mchezo wa kwanza Bayern imempiga Barcelona 4-0 na mchezo wa pili pale Camp Nou Bayern ikamkausha tena mabao 3-0 hii ilikuwa mwaka 2012.
1.AC MILAN DHIDI YA BARCELONA
Mchezo wa fainali sasa ambapo AC Milan amepiga Barcelona mabao 3-0 na kuchukua ubingwa katika orodha hii Ac Milan imeingia sana wakati huo ilikuwa inasumbua sana.
Je wewe yako ipi ambayo umeona ilikuwa inatikisa na ilikuvutia kwa kufunga magoli mengi .
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
Bonyeza Hapa CLICK HERE
0 comments:
Post a Comment