Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amemuandikia waraka Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli akimsihi kuruhusu
kufanyika kwa mikutano ya kisiasa nchini bila kujali mipaka ya majimbo.
Lema
amepaza sauti yake kupitia waraka wake kwa Rais Magufuli, uliosambazwa
kwenye mitandao ya kijamii, waraka ambao alithibitisha kuwa ni wake.
Katika
waraka huo, Lema ambaye pia na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,
alimsihi Rais Magufuli kuviruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano hiyo
kwani ni sehemu ya matakwa ya katiba.
Alitahadharisha
kuwa endapo mambo yaliyoruhusiwa kikatiba hayataruhusiwa, ipo siku amri
za utekelezaji wa masuala muhimu kikatiba hazitachukuliwa kwani
hakutakuwa na sababu ya kuheshimu katiba na utawala wa sheria.
“Kama
hatuwezi kufanya tunayoruhusiwa na Katiba, na anayetuzuia mamlaka yake
yametokana na Katiba, hakika mbegu inayopandwa ni hatari kwa ustawi wa
Taifa, ipo siku amri ya utekelezaji juu ya masuala muhimu haitachukuliwa
kwa sababu umuhimu wa kuheshimu katiba na utawala wa Sheria
hautakuwepo,” aliandika.
Lema
alimueleza Rais Magufuli kuwa Siasa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine
na kwamba mfumo huo ndiyo chanzo cha madaraka waliyonayo hapa nchini.
“Mheshimiwa
Rais, siasa ni kazi na ndiyo maana wewe ni rais kwa sababu ya siasa, na
mimi ni mbunge kwa sababu ya siasa, tena ni kazi muhimu sana tu kwani
ndio mfumo pekee unaotafuta utawala wa ngazi mbalimbali na wa juu kabisa
katika nchi,”
Aidha,
Lema alimsemea kwa Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekitiwa CCM, Msemaji wa
chama hicho, Christopher Ole Sendeka kwa kukiuka amri aliyoitoa Rais
kwa kufanya mkutano Longido ambako sio jimbo lake.
“Mheshimiwa
Rais, jambo hili litaleta mpasuko katika taifa letu, ni kauli
inayopaswa kurekebishwa haraka. Hivi karibuni, msemaji wa CCM, Ole
Sendeka alifanya mkutano Longido. Je, Ole Sendeka ni Mbunge wa Longido?
Au polisi wa Mkoa wa Arusha hawakusikia tamko lake? " Alihoji.
Mbunge
huyo alisisitiza kuwa Chadema itafanya maandamano Septemba Mosi mwaka
huu, huku akihoji madhara yanayoweza kujitokeza siku hiyo, hivyo
akamuomba Rais kutengua amri yake ya kuzuia mikutano ya hadhara
0 comments:
Post a Comment