Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>Hali Ngumu ya Maisha, Afisa wa Polisi Ajiua Kwa Kujipiga Risasi Jomo Kenyatta (JKIA).Fahamu zaidi hapa.
Afisa wa polisi Caudencia Wausi alimejiua kwa kujipiga risasi kichwani
katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) muda mfupi baada ya
kuchapisha ujumbe wa kuashiria kuwa na mahangaiko maishani.
Koplo Caudencia Wausi alitumia bastola yake aina ya Jericho kujifyatulia
risasi kichwani ndani ya choo dakika 13 tu baada ya kuchapisha ujumbe
katika mtandao wake wa Facebook.
"Maisha ni magumu unapoishi katika ulimwengu ambapo kila mtu anapanga
kukufanyia maovu.. na utafanya nini wakati ambapo huwezi kuvumilia au
hauna uwezo wa nguvu za kuwatia nguvu wapendwa wachache katika maisha
yako.!? hauna lingine la kufanya ila... kwa hivi nisadie Mungu
"aliandika kwenye Facebook.
Kwa mujibu wa mkubwa wake, Bi Wausi alikuwa amerudi kazini kutoka mapumzikoni kabla ya kujiua baada ya kujifungia chooni, JKIA.
Inadaiwa alijifungua mkanda wake wa polisi na kuuacha katika chumba cha
Control Room pamoja na fimbo yake kabla ya kujifungia chooni.
"Tulisikia tu mlio wa risasi na baadaye tukampata juu ya choo huku
bastola yake ikiwa mkononi, alikuwa tayari ameaga dunia "alisema kamanda
wa polisi katika uwanja wa ndege Rono Bunei.
Bwana Bunei alisema kisa hiki kimeshtua wenzake kwasababu afisa huyo hakuwa na dalili za kusongwa na mawazo.
" Alikuwa anapiga gumzo na wenzake asubuhi na nilimuona mwenye furaha,
hakuonyesha dalili zozote za kuwa na mahangaiko "alisema Bw Bunei na
kuongeza kuwa uchunguzi umeanza kubaini kilichosababisha afisa huyo
kujiua.
Related Posts:
Makonda atangaza vita nyingine, “hawa ni halali yangu”.Fahamu zaidi hapa.
Siku chache baada ya kutangaza vita dhidi ya dawa za kulevya na
kuanza kuitekeleza kwa kasi, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
ametangaza vita mpya na makandarasi wasio wawajibikaji.
Makonda ametangaza vita hi… Read More
Tanesco Yatoa Tahadhari Hii Kufuatia Mvua Zinazonyesha...!!!.Fahamu zaidi hapa.
Shirika la umeme Tanzania (TANESCO),limetoa tahadhari kwa wateja wake na
wananchi kwa ujumla juu ya mvua zinazonyesha. Miongoni mwa tahadhari
hiyo ni pamoja kutofanya biashara katika miundo mbinu ya umeme.
Down… Read More
Keko, Dar: Teja Afariki na Bomba la Sindano ya Madawa ya Kulevya Mkononi...!!!.Fahamu zaidi hapa.
Hapa DDC Keko, Dar es salaam, kwenye eneo la wazi, katika ukuta
unaotenganisha eneo hilo na National Hotel, wakazi wamekusanyika kwa
tahayuri baada ya kumuona kijana amelala ukutani na hapumui, inaonekana
ameshakufa mud… Read More
Kazi Imeanza..Ridhiwani Kikwete Ahojiwa na Tume Dawa za Kulevya, Asema Haya...!!!.Fahamu zaidi hapa.
Mbunge wa Chalinze jana alihojiwa na tume ya kupambana na kudhibiti
madawa ya kulevya. Alipoulizwa kuhusu kuitwa huko, mwenyekiti wa tume
hiyo, jaji Siang'a amesema kila aliyetajwa kwenye orodha ya wanaohusika
ataitwa. N… Read More
Dr. Makongoro Mahanga Atoweka.....Polisi Waendelea Kumsaka.Fahamu zaidi hapa.
Aliyekuwa
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Makongoro
Mahanga, anayesakwa na Jeshi la Polisi ametoweka nyumbani kwake.
Mahanga
anasakwa na polisi kutokana na amri ya Mahakama Kuu Kanda ya … Read More
0 comments:
Post a Comment