TEVERAS
Kocha
wa African Lyon, Mreno, Bernardo Teveras, ameibuka na kusema kuwa
anahitaji matokeo ya ushindi katika mchezo wake wa pili wa Ligi Kuu Bara
dhidi ya Yanga kwa kuwa alishawaona walipocheza na Azam FC, hivi
karibuni.
Mreno
huyo amechukua nafasi ya kocha wa zamani wa Simba aliyekuwa akiinoa
timu hiyo, Dragan Popadic raia wa Serbia aliyeondoka nchini kutokana na
madai ya vyeti vyake kuwa ni vya kizamani na havifai katika soka la
sasa.
Tavares
amesema kuwa kwa sasa akili yake ameielekeza katika mchezo dhidi ya
Yanga kwa ajili ya kujiwekea mazingira mazuri katika ligi.
“Tulikuwa
na wakati mzuri katika mchezo wetu dhidi ya Azam, japokuwa wapinzani
wetu walipata nafasi ya kusawazisha dakika za mwisho, kwa sasa mipango
yangu naielekeza katika mchezo wetu ujao dhidi ya Yanga kwani nahitaji
ushindi kutoka kwao.
"Uzuri
ni kwamba Yanga tayari nimeshawaona walipocheza mchezo wa Ngao ya Jamii
dhidi ya Azam kwani ni timu nzuri na ya gharama, lakini ninachokitaka
ni ushindi pekee licha ya muda mchache ambao nimekaa nayo ila imani
yangu ni kuwafunga tu, hakuna kingine," alisema Tavares.
African Lyon ilionyesha soka safi na kuibana Azam FC katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.
0 comments:
Post a Comment