WAZIRI
wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye amezifungia
radio mbili kwa muda usiojulikana kwa makosa ya kuandaa vipindi ambavyo
vimerushwa hewani vinavyoashiria uchochezi.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Waziri Nape amesema kuwa uamuzi wa kuvifungia
vituo hivyo umefikiwa baada ya kujirdhisha kuwa kipindi cha Matukio
kilichorushwa Agosti 25, 2016 muda wa saa 2 usiku hadi saa 3 na kituo
cha utangazji cha Radio 5 pamoja na kipindi cha Morning Magic katika
kipengele cha Kupaka Rangi Agosti 17 vilikuwa na maudhui ya uchochezi
unaoweza kuleta uvunjifu wa Amani.
Nape
amesema kuwa kufuatia hilo amevifungia kwa muda usiojulikana kwani
wamekiuka masharti ya kanuni ya 5 (a, b, c na d) , kanuni ya 6 (2a, b na
c) na kanuni ya 218 ya huduma za utangazaji ya mwaka 2005.
Wakati
vituo hivyo vikifungiwa kwa muda usiojulikana kamati ya maudhui imepewa
jukuu la kuviita na kusikiliza kwa kina Zaidi utetezi wao na ni hatua
gani zaidi ya kuchukua dhidi yao kwa mujibu wa kanuni ya huduma za
utangazaji.
Nape
ameendelea kuvitahadhalisha vyombo mbalimbali vya habari kutoshawishika
kuvunja sheria na kanuni zinazoongoza tasnia ya habari ili kulinda
heshima ya tasnia yetu na wakati huo kuhakikisha nchi inabaki na Amani,
Mshikamano na Umoja.
0 comments:
Post a Comment