Home »
Habari Moto
» #YALIYOJIRI>>>>JAJI WARIOBA AAMUA KUMJIBU HIVI MZEE KINGUNGE.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Siku moja baada ya Mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru
kuwaomba viongozi wastaafu kumshauri Rais John Magufuli kuikutanisha
Serikali na Chadema ili kuvunja UKUTA kwa amani, Jaji Joseph Warioba
amejibu.
Jaji Warioba amesema kuwa suala hilo lisichukuliwe kama tatizo la Rais John Magufuli pekee bali ni tatizo la watu wote nchini.
“Ni wajibu wa Watanzania wote kuhakikisha wanalinda hali ya amani
nchini badala ya kuliona hilo… kusema jambo hili halimhusu Rais John
Magufuli pekee, linamhusu mtu mwingine yeyote. Tumsaidie msajili katika
hili, hili sio tatizo la mtu mmoja bali ni la nchi nzima, tusimuachie
Rais wetu,” Jaji Warioba amekaririwa.
Amesema kuwa badala ya kumjibu Mzee Kingunge, ni vyema kumpa nafasi
Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kuwakutanisha
viongozi wa vyama vya siasa ili kujadili kwa lengo la kutafuta muafaka.
Aidha, Jaji Warioba alisema kuwa wao kama wazee wamekuwa wakimshauri
Rais kwa mambo mengi, lakini ushauri huo hawautoi kupitia vyombo vya
habari.
“Kweli tuko kimya lakini ukimya huo usitafsiriwe vibaya kuwa
hatumshauri Rais Magufuli, sisi kama viongozi wastaafu tunamshhauri rais
lakini sio katika vyombo vya habari,” alisema
Related Posts:
Nyumba 100 Chalinze zaharibiwa na mvua.Fahamu zaidi hapa.
MKUU
wa Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani Majid Mwanga, amesema nyumba zaidi
ya nyumba 100 zilizopo Kata za Bwilingu eneo la Chalinze Mzee na Msoga
zimeharibika na nyingine kuezuliwa mapaa kutokana na mvua zinazoen… Read More
Mfumuko wa Waongezeka kwa Asilimia 1.4..Sasa Umefikia Asilimia 6.4.Fahamu zaidi hapa.
Kiwango cha mfumuko wa bei nchini kimepanda kwa wastani wa 1.4 kutoka
asilimia 5 ilivyokuwa mwezi Februari hadi asilimia 6.4 kwa mujibu wa
taarifa kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini (NBS).
Kwa mujibu wa taarifa h… Read More
Mbunge wa Chemba Juma Nkamia Amshangaa Mwakyembe Kuhudhuria Press Conference ya Roma.Fahamu zaidi hapa.
Mbunge wa Chemba Juma Nkamia (CCM) amemshangaa Waziri wa Waziri wa
Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Mwakyembe kuhudhuria press
conference
Binafsi ya Msani Roma Mkatoliki,na kusema kuwa kitendo hicho kinazidisha masw… Read More
Bashe: CCM Acheni Unafiki, Mimi Nimeshakamatwa na Watu wa Usalama. Nipo Tayari Mniondoe Kwenye Chama Chenu.Fahamu zaidi hapa.
Mbunge HusseinBashe awataka wabunge CCM kuacha unafiki, akisema yupo
tayari kufukuzwa ila kweli alikamatwa na maafisa wa usalama wa taifa.
'CCM acheni unafiki mimi nimeshakamatwa na watu wa usalama mnasema hawakamati, … Read More
#BREAKING NEWZ>>>KIJANA AKATWA MKONO KISA DENI LA 300,000 HUKO TARIME.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Mkazi
wa Kijiji cha Keisangora, Wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Mwita Magige,
amekatwa mkono wa kushoto kwa kile kinachodaiwa kushindwa kulipa deni la
sh 300,000 baada ya ng’ombe wake wane kukamatwa na mdeni wake.
Tukio… Read More
0 comments:
Post a Comment